Waziri
wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe ametangaza
nia ya kuwania nafasi ya urais wa serikali ya awamu ya 5, huku akisema
ikiwa akipata ridhaa ya watanzania kwenye uchaguzi mkuu ujao kipaumbele
chake kitakuwa kuboresha kilimo na viwanda, usalama wa raia, afya, elimu
na kushirikiana na sekta binafsi katika kukuza uchumi wa taifa.
Akitangaza nia hiyo mjini Lindi Mheshimiwa Membe amesema amejipima
na kujiona ana uwezo wa kuitumikia nafasi hiyo ya urais kwa kuwa ana
elimu nzuri na uzoefu wa kazi katika serikali na chama ukulinganisha na
wagombea wengine wanaowania nafasi hiyo ndani ya CCM.
Aidha mbali na kuahidi serikali yake itahakikisha huduma za afya
zinawafuata wananchi badala ya ilivyo sasa wananchi kuifuata huduma
hizo, amesema ataipeleka nchi hii kwenye uchumi wa viwanda utakaobeba
kilimo kutokana na ugunduzi wa gesi nchini.
Akizungumzia usalama wa taifa, Mheshimiwa Membe amesema akabiliana
kikamilifu na maovu katika jamii ikiwemo mauaji ya watu wenye ulemavu wa
ngozi albino, tishio la ugaidi, madawa ya kulevya na ujambazi na kutuma
salama kwa wanaojihusishja na vitendo hivyo, kuacha mara moja kabla
yeye hajaingia madarakani.
No comments:
Post a Comment