MWANADIPLOMASIA maarufu, Balozi Dk Augustine Mahiga ametangaza nia
kukiomba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumfikiria na hatimaye kupendekeza
ili apate fursa ya kugombea nafasi ya Urais wa Tanzania.
Dk Mahiga pamoja na nia yake amekuja na vipaumbele vyake kuwa ni kuleta umoja, amani na maadili, kupambana na rushwa na ufisadi, kukuza uchumi na kuimarisha uhusiano wa kimataifa.
Akitangaza nia jana mbele ya waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), alisema ameamua kuchukua hatua hiyo kwa kuwa ni haki yake, lakini pia amepata fursa ya kuielewa nchi yake, dira, uchumi, siasa na utamaduni wake na kuitangaza ndani na nje ya nchi.
“Ningependa kusimama na kugombea nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia CCM katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu. Nimetafakari muda mrefu na nikafikia muafaka wa kujitosa katika kinyanganyiro hiki, naomba nifikiriwe na hatimaye kupendekezwa na kupata fursa ya kuongoza taifa hili,” alisema.
Afafanua vipaumbele vyake Akifafanua vipaumbele hivyo, alisema misingi ya taifa hili inahitaji kuimarishwa na kusimamiwa na ili kufanikisha hilo lazima umoja uliopo uendelee kudumishwa kwani ndio nguvu iliyosaidia kumtoa mkoloni, kuondoa udini, ukabila, ukanda na masuala ya rika.
Katika suala hilo la umoja, pia alisema vyama vya siasa vinapaswa kuishi katika utamaduni wa vyama vingi, ambao ni kupanuka kwa demokrasia na kwamba ushindani wa kisiasa usiwe mapambano, ila vyama vya siasa vinapaswa kufanya kazi kwa pamoja.
Akizungumzia msingi wa maadili, alisema ndani yake kuna uzalendo, uadilifu, uwajibikaji na ukweli na kwamba hayo ni muhimu katika jamii na utawala na uongozi bora na kuongeza kuwa maadili yanapaswa kujengwa na Watanzania wasiogope kujikosoa.
Alisema mambo yanayohitaji kushughulikiwa haraka katika maadili ni rushwa na ufisadi kwa sababu vimeleta madhara makubwa kisiasa na kiuchumi na katika kuheshimika kimataifa.
Balozi Mahiga alisema vita dhidhi ya rushwa na ufisadi, inahitaji utashi wa kisiasa na uratibu mzuri wa vyombo na mamlaka husika, zinazoshughulikia masuala hayo, watu washirikishwe wakiwemo watu wa kawaida kusema kwa kile alichoeleza wanajua mambo mengi.
Akizungumzia uchumi alisema unatakiwa uchumi unaowiana na mahitaji ya Watanzania kuanzia tabaka la chini, ukizingatia taifa linaelekea kwenye uchumi wa kati.
Mahiga ni nani?
Awali akijitambulisha kwa Watanzania kupitia vyombo vya habari, Balozi Mahiga aliyeambatana na mkewe Elizabeth Mahiga, mtoto wake wa kiume Maliva Mahiga, Katibu wa zamani wa Bunge na Mbunge wa zamani wa Kalenga, George Mlawa na Mhandisi Marcus Chogo, alisema yeye ni Mtanzania aliyesoma Tanzania hadi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Kisha alikwenda kusoma nje ya nchi katika Chuo Kikuu cha Toronto, Ontario nchini Canada, alipopata Shahada mbili za Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.
Alisema kisha alirudi UDSM, ambapo alikuwa mhadhiri kwa miaka miwili katika Idara ya Siasa na kisha wakati huo ukiwa Utawala wa Baba wa Taifa, Julius Nyerere alipelekwa na kujiunga na Idara ya Usalama, ambapo alifanya kazi kwa miaka mitatu kama Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa.
Alisema kilikuwa kipindi cha harakati za ukombozi wa nchi za Afrika kwa hiyo idara yake ilishughulika vilivyo. Lakini pia wakati wa Vita vya Kagera vya kumuondoa Iddi Amini alipata fursa ya kuelewa nchi na chimbuko na fikra za waasisi, akiwepo Mwalimu Julius Nyerere.
Balozi Mahiga alisema ukiwa ndani ya idara ya usalama hakuna jambo usilolijua, hivyo anakifahamu chama, dira, uchumi , siasa na utamaduni wa taifa hili na kwamba anaweza kuwa mshauri mzuri wa chama na serikali.
Dk Malecela, Dk Kigwangala wachukua fomu
WAGOMBEA wa Urais wawili jana walichukua fomu akiwemo Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Dk Mwele Malecela na Mbunge wa Nzega, Dk Nasser Kingwangala ambaye alisema hatumii fedha nyingi kwenye kampeni kwa kuwa hahongi.
Dk Mwele anakuwa mwanamke wa pili kuwania nafasi hiyo, ambapo mwanamke mwingine aliyechukua fomu ni Balozi Amina Salum Ally. Alisema CCM imekuwa ikitoa nafasi sawa kwa watu wote, amejipima, ametafakari na ameomba na kuona anafaa kuwa mgombea katika nafasi hiyo hali iliyomsukuma kuchukua fomu kuomba ridhaa.
Alisema kikubwa kilichomsukuma ni kiu yake ya kutaka kuwatumikia Watanzania, kwani amefanya sana kazi na jamii na sasa ni wakati wake wa kuleta mabadiliko.
“Tulianza na Baba wa Taifa ambaye alijenga uzalendo, watu kupendana na kujaliana, wakati wa Mzee Mwinyi kulikuwa na mabadiliko ya uchumi, wakati wa Rais Mkapa kulikuwa na mabadiliko ya kimfumo na kwenye serikali ya Rais Kikwete kuna mabadiliko makubwa ya miundombinu,” alisema Dk Mwele alisema endapo atapitishwa na CCM, atatoa msukumo kwenye elimu ya ufundi na kuwajenga vijana kutoka walipo na kuwaingiza kwenye soko la ajira.
Akizungumzia uchumi, alisema ataimarisha mifumo iwe na tija kwa taifa huku akiahidi kuendeleza na kulinda muungano. “Sasa Tanzania inakuwa na matabaka kati ya matajiri na maskini, rabsha za dini na ukabila hazijengi. Alisema serikali ya awamu ya nne imewainua sana wanake kuwa viongozi katika nafasi za serikali na hata siasa.
Aliahidi kupambana na rushwa na kuleta mfumo wa uwajibikaji na anataka kuipeleka heshima ya sayansi kwenye siasa. “Nimelelewa kwenye nyumba ya mwanasiasa si wakati wote ni longolongo kuna mambo mengi mazuri,” alisema.
Dk Hamis Kingwangala
Alisema atapunguza baraza la mawaziri ili kuwa na mawaziri wachache watendaji.
“Jambo la kwanza ni kuwa na watu wa kufanya nao kazi na nitapunguza Wizara kuna watu wamekaa hawana maisha bila kujali hakuna kinachoendelea na kikiharibika wa kwanza kutukanwa nia Rais,” alisema.
Alisema kati ya mambo atakayofanya ni kupunguza ukubwa wa serikali atakuwa na mawaziri wachacche ambao wanafanya kazi. “Wakikuona uko makini na unapima matokeo kila mtu atafanya kazi, ukiona kuna viongozi wanaopimwa na wao watakuwa wakali kwa wale wa chini yao” alisema.
Alisema iwapo atachaguliwa kuongoza nchi lazima atakuwa na mipango ya muda mfupi na muda mrefu, kuna mambo ya kutekeleza leo na yake ya baadae kuna usalama wa chakula, elimu, umeme na barabara.

No comments:
Post a Comment