Dolores Aveiro, alikua katika uwanja wa ndege wa mjini Madrid, Barajas wakati polisi walipomfanyia ukaguzi na kugundua kuwa alikua na Euro elfu 55.
Mtu huruhusiwa kuchukua kiasi cha Euro elfu 10 na kusafiri nazo lakini mama yake Christiano alizidisha mara tano ya kiwango hicho.
Kutokana na kushindwa kutoa sababu iliyomfanya abebe kiasi kikubwa cha pesa, polisi walichukua euro elfu 45 na kumruhusu kuingia na euro elfu 10 tu.
Aveiro, atapigwa faini ili kuweza kuzichukua pesa zilizosalia uwanja wa ndege.
No comments:
Post a Comment