Monday, 30 June 2014

Podolski nje ya mechi dhidi ya Algeria

Podolski na Boateng katika orodha ya majeruhi ya Ujerumani
Mshambulizi wa Ujerumani na Arsenal ya Uingereza Lukas Podolski hatoweza kushiriki mechi ya mkondo wa pili kati ya Ujerumani na Algeria iliyoratibiwa kuwa Porto Alegre.
Mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 29 ambaye anashiriki kombe lake la tatu la dunia inasemekana kuwa alijeruhiwa katika mechi yao ya mwisho ya makundi dhidi ya Marekani .
Sasa madaktari wa timu hiyo inayopigiwa upatu kufuzu kwa fainali ya kombe la dunia mwaka huu wanasema kuwa anahitaji angalau siku mbili au tatu kupumzika ilipaja lipate nafuu na hiyo inamaanisha kuwa kocha Joachim Loew
sasa atalazimika kumchezesha mshambulizi mwengine upande wa kushoto .
Podolski na Boateng katika orodha ya Majeruhi ya Ujerumani
Kutokuwepo kwa Podolski sasa kutampatia mshambulizi wa Bayern Munich ya Ujerumani Mario Goetze nafasi ya kutawala dhidi ya Algeria.
Kikosi cha Loew kingali kinasuri habari kumhusu kiungo wa upande wa kulia Jerome Boateng ambaye pia hakuweza kushiriki mazoezi yao ya mwisho kutokana na jeraha la goti.
Ujerumani itachuana na the Desesrt Foxes ya Algeria jumatatu katika uwanja wa Porto Alegre’s Beira-Rio

Pistorius hakuwa na tatizo lolote la kiakili wakati alipomuua mpenzi wake

Pistorius amekana madai ya kuua mpenzi wake kwa maksudi
Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius hakuwa na tatizo lolote la kiakili wakati alipomuua mpenzi wake mwaka jana.
Haya ni matokeo ya uchunguzi wa kiakili aliofanyiwa Oscar Pistorius huku kesi yae ikianza kusikilizwa tena nchini Afrika Kusini.
Ripoti hiyo iliwasilishwa baada ya uchunguzi kufanywa kuhusu hali yake ya kiakili wakati alipofanya mauaji hayo mwaka jana.
Mawakili wake walikuwa wamedai kuwa Pistorius aliukuwa anakumbwa na hali ya wasiwasi na kuzongwa na mawazo wakati wa mauaji ya Reeva Steenkamp.
Mwanariadha huyo amekana kumuua kwa maksudi mpenzi wake Reeva Steenkamp akisema kuwa alimpiga risasi kwa bahati mbaya baada ya kupatwa na wasiwasi akidhani jambazi alikuwa amevamia nyumba yake.
Upande wa mashitaka pamoja na utetezi wamekubali matokeo ya uchunguzi huo.
Upande wa utetezi sasa unasikia ushahidi wake daktari aliyemkata miguu Pistorius, Gerry Versfeld, anayetoa ushahidi kuhusu athari za Pistorius kukatwa miguu.
Upande wa utetezi nao unatarajiwa kumaliza ushahidi wake katika siku chache zijazo.
Bi Steenkamp, alikuwa na umri wa miaka 29, wakati wa mauaji yake Februari mwaka jana.

Sunday, 29 June 2014

Evance Eveva raisi mpya Simba sc

109UCHAGUZI mkuu wa klabu ya Simba sc umemalizika salama licha ya changamoto kadhaa kujitokeza na sasa zoezi linaloendelea ni kumalizia kuhesabu kura za wagombea wa nafasi za ujumbe.
Kwa nafasi ya Urais, tayari mambo yameshafahamika ingawa taarifa rasmi kutoka kamati ya uchaguzi haijatangazwa.
Evans Elieza Aveva ni rais wa kwanza wa klabu ya Simba kwani matokeo ambayo sio rasmi yanaonesha ameibuka na ushindi mkubwa.
Aveva amepata kura 1461, huku mpinzani wake pekee, Andrew Peter Tupa akipata kura 381.
Wagombea hawa walikuwa na uzito tofauti, kwasababu dalili za Eveva kushinda zilianza siku aliyoenda kuchukua fomu.
Hata hivyo ilionekana kungekuwa na mchuano mkali endapo Michael Richard Wambura angeendelea na uchaguzi.
Nafasi ya makamu wa rais, aliyewahi kuwa makamu mwenyekiti wa Simba katika uongozi unaomaliza muda wake, Geofrey Nyange `Kaburu` kwa matokeo yasiyo rasmi ameshinda nafasi hiyo.
Matokeo rasmi yatatangazwa muda wowote kutoka sasa, endelea kufuatilia mtandao huu.
109
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
UCHAGUZI mkuu wa klabu ya Simba sc umemalizika salama licha ya changamoto kadhaa kujitokeza na sasa zoezi linaloendelea ni kumalizia kuhesabu kura za wagombea wa nafasi za ujumbe.
Kwa nafasi ya Urais, tayari mambo yameshafahamika ingawa taarifa rasmi kutoka kamati ya uchaguzi haijatangazwa.
Evans Elieza Aveva ni rais wa kwanza wa klabu ya Simba kwani matokeo ambayo sio rasmi yanaonesha ameibuka na ushindi mkubwa.
Aveva amepata kura 1461, huku mpinzani wake pekee, Andrew Peter Tupa akipata kura 381.
Wagombea hawa walikuwa na uzito tofauti, kwasababu dalili za Eveva kushinda zilianza siku aliyoenda kuchukua fomu.
Hata hivyo ilionekana kungekuwa na mchuano mkali endapo Michael Richard Wambura angeendelea na uchaguzi.
Nafasi ya makamu wa rais, aliyewahi kuwa makamu mwenyekiti wa Simba katika uongozi unaomaliza muda wake, Geofrey Nyange `Kaburu` kwa matokeo yasiyo rasmi ameshinda nafasi hiyo.
Matokeo rasmi yatatangazwa muda wowote kutoka sasa, endelea kufuatilia mtandao huu.
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=2861#sthash.WgrMGVv0.dpuf
109
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
UCHAGUZI mkuu wa klabu ya Simba sc umemalizika salama licha ya changamoto kadhaa kujitokeza na sasa zoezi linaloendelea ni kumalizia kuhesabu kura za wagombea wa nafasi za ujumbe.
Kwa nafasi ya Urais, tayari mambo yameshafahamika ingawa taarifa rasmi kutoka kamati ya uchaguzi haijatangazwa.
Evans Elieza Aveva ni rais wa kwanza wa klabu ya Simba kwani matokeo ambayo sio rasmi yanaonesha ameibuka na ushindi mkubwa.
Aveva amepata kura 1461, huku mpinzani wake pekee, Andrew Peter Tupa akipata kura 381.
Wagombea hawa walikuwa na uzito tofauti, kwasababu dalili za Eveva kushinda zilianza siku aliyoenda kuchukua fomu.
Hata hivyo ilionekana kungekuwa na mchuano mkali endapo Michael Richard Wambura angeendelea na uchaguzi.
Nafasi ya makamu wa rais, aliyewahi kuwa makamu mwenyekiti wa Simba katika uongozi unaomaliza muda wake, Geofrey Nyange `Kaburu` kwa matokeo yasiyo rasmi ameshinda nafasi hiyo.
Matokeo rasmi yatatangazwa muda wowote kutoka sasa, endelea kufuatilia mtandao huu.
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=2861#sthash.WgrMGVv0.dpuf
109
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
UCHAGUZI mkuu wa klabu ya Simba sc umemalizika salama licha ya changamoto kadhaa kujitokeza na sasa zoezi linaloendelea ni kumalizia kuhesabu kura za wagombea wa nafasi za ujumbe.
Kwa nafasi ya Urais, tayari mambo yameshafahamika ingawa taarifa rasmi kutoka kamati ya uchaguzi haijatangazwa.
Evans Elieza Aveva ni rais wa kwanza wa klabu ya Simba kwani matokeo ambayo sio rasmi yanaonesha ameibuka na ushindi mkubwa.
Aveva amepata kura 1461, huku mpinzani wake pekee, Andrew Peter Tupa akipata kura 381.
Wagombea hawa walikuwa na uzito tofauti, kwasababu dalili za Eveva kushinda zilianza siku aliyoenda kuchukua fomu.
Hata hivyo ilionekana kungekuwa na mchuano mkali endapo Michael Richard Wambura angeendelea na uchaguzi.
Nafasi ya makamu wa rais, aliyewahi kuwa makamu mwenyekiti wa Simba katika uongozi unaomaliza muda wake, Geofrey Nyange `Kaburu` kwa matokeo yasiyo rasmi ameshinda nafasi hiyo.
Matokeo rasmi yatatangazwa muda wowote kutoka sasa, endelea kufuatilia mtandao huu.
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=2861#sthash.WgrMGVv0.dpuf

JK asemema UKAWA watatufanya tuendelee kutumia katiba ya 1977

Wakati kukiwa na juhudi za watendaji wa Bunge maalumu la Katiba kuwashawishi viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani wawaruhusu wabunge wao kurejea bungeni wakati vikao vya Bunge hilo vitakavyoanza Agosti 5 mwaka huu, bado utata umegubika kuhusu uwezekano wa kupatikana katiba hiyo kwa wakati
Hata hivyo tayari Rais Jakaya Kikwete amesema kuwa kama katiba hiyo haitapatikana sasa, Katiba ya Muungano mwaka 1977, itaendelea kutumika.
Kwa wakati, siku na mara kadhaa zimefanyika juhudi hizo bila ya kuzaa matunda, huku viongozi wa vyama vya CUF, Chadema na NCCR-Mageuzi, wakionekana kuweka ngumu na kutoa masharti kwa Serikali kama itataka warejee bungeni.
Ni dhahiri sasa msimamo huo umeendelea kuliweka taifa katika wakati mgumu hasa inapoonekana kuwa matumaini ya kupata Katiba Mpya yanaendelea kufutika.
Katibu wa Bunge Maalumu la Katiba Yahya Khamis Hamad anatoboa siri ya Bunge kuchukua juhudi hizo na kusema hata hivyo bado hazijazaa matunda na hadi sasa bado haijafahamika kama wabunge wa kundi a Ukawa watarajea au la.
Hamad anazitaja baadhi ya hatua zilizochukuliwa hadi sasa kuwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Bunge la Katiba Samuel John Sitta kukutana na viongozi wa vyama hivyo kwa nyakati tofauti, akiwamo Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad mwenye ushawishi mkubwa kwenye kundi la Ukawa.
Aidha, chama cha CUF ndicho chama chenye Wawakilishi wengi katika Bunge la Katiba baada ya kuwa na wabunge wa kuchaguliwa, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na wa kuteuliwa.
Akiwa Zanzibar, Sitta pia amekutana na Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein chini ya agenda hiyo akihimiza na kuwataka wajumbe hao kurejea na kuhitimisha ng’we iliyobaki.
Katibu wa Bunge la Katiba Mpya anabainisha kuwa matayarisho ya Mkutano wa Pili wa Bunge maalumu la Katiba yameanza kufanyika na kikao cha kwanza kinatarajiwa kuanza Agosti 5 mwaka huu, huku wakiwa na matumaini kuwa kundi la Ukawa litarejea na kushiriki vikao vya Bunge hilo.
Hamad anasema milango iko wazi kwa wabunge hao kurejea na kushiriki Bunge hilo ili kusaka suluhu kupitia kamati ya uongozi pamoja na ile ya maridhiano na kufikia mwafaka wa mvutano uliojitokeza badala ya kundi hilo kubaki nje ya Bunge.
Katibu huyo anaeleza kuwa haamini kama kuendelea kwa Ukawa kubaki nje ya Bunge ni njia sahihi na ya uhakika, badala yake angetamani warudi bungeni ili madai hayo yakafanyiwe kazi.
Pia amesema hatua ya wabunge wengi wa makundi maalumu miongoni mwa 201 kuendelea kubakia kwenye Bunge, ni jambo linalotia faraja na matumaini kama njia inayoweza kurahisisha kupata theluthi mbili ya wabunge wa Bunge hilo.
Kwa maoni na mtazamo wake, Hamad anasema kuondoka kwa wabunge wa kundi la Ukawa hakujaathiri kutoendelea kufanyika kwa vikao vya Bunge hilo ila kikwazo kitabaki katika upatikanaji wa theluthi mbili za uamuzi wa vikao vya Bunge hilo kwa mujibu wa kanuni zilizopo.
Hamad anasema ikiwa hali ya kukosekana theleluthi mbili itajitokeza, hakuna njia nyingine mbadala zaidi ya Katiba ya Nchi ya mwaka 1977 kuendelea kutumika ikiwamo suala la mfumo wa serikali mbili kuendelea kutumika na kukwama kwa utatuzi wa baadhi ya kero katika Muungano.
Lipumba atoa neno
Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba ameuambia Mkutano Mkuu wa CUF kwamba kundi la Ukawa litakuwa tayari kurejea bungeni ikiwa Rais Jakaya Kikwete atawaomba radhi Watanzania kwa kupuuza maoni yao katika mchakato wa katiba. Profesa Lipumba alisema ili Ukawa warejee bungeni na kushiriki vikao, Rasimu ya Mwenyekiti Jaji Joseph Warioba isipanguliwe.
CCM imeshawishi na kufanikiwa kutupa baadhi ya vipengele kwenye rasimu hiyo ikieleza kuwa siyo msaafu, Biblia au Sheria ya nchi, anasema Profesa Lipumba.
ZEC: Hatujafanya matayarisho kura ya maoni
Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC) Salum Kassim Ali anasema ZEC haijaanza matayarisho yoyote ya kura ya maoni kwa upande wa Zanzibar kutokana na kile alichodai kutanda kwa giza nene usoni mwa jambo hilo.
Salum amesema huwezi kuanza kufanya matayarisho ya jambo kubwa kama hilo, huku ikionekana hakuna jambo la msingi linalofanyika bungeni.
“Tunaweza kufanya matayarisho ya kura kama kutakuwa na dalili njema ya kupita kwa rasimu na siyo kama ilivyo sasa,” anasema.
Amesema ZEC inahitaji muda wa matayarisho ya jambo hilo ikiwa ni pamoja na utoaji wa elimu ya uraia kwa upana wa kutosha kwa wananchi na kukosoa mchakato wa kuitishwa kura ya maoni mwaka 2009 ulikuwa ni wa lipualipua na kukosa maandalizi ya kutosha ya jambo hilo.
Baadhi ya wakazi wa Zanzibar wameendelea kugawanyika, huku wengine wakieleza kuwa kutopita kwa katiba hiyo, kunaweza kuendelea kuikwamisha zaidi Zanzibar kujitanua kiuchumi.
Wamesema katiba hiyo haitakuwa na maana kama haitaheshimu kilio cha muda mrefu Wazanzibari cha Zanzibar na mamlaka kamili.

Vijiji na makanisa ya shambuliwa tena Nigeria


Shule ya Chibok ambapo wanafunzi wasichana walitekwa nyara ApriliWatu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Boko Haram wameshambulia vijiji kadha na makanisa kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Wakaazi wa huko walisema kuwa watu wengi wameuwawa na nyumba nyingi zimeteketezwa.
Mashambulio yamefanywa karibu na mji wa Chibok, ambako wasichana wa shule zaidi ya 200 walitekwa nyara mwezi wa Aprili.
Mwandishi wa BBC Nigeria anasema katika kijiji kimoja cha Kautikari, wanamgambo wa kijiji walizidiwa nguvu walipojaribu kulinda kanisa.
Anasema jeshi halikuweza kufika katika vijiji hivyo vilioko mbali.

Friday, 27 June 2014

Jasmin Sudi awaomba wanachama wa Simba wamchague

Mgombea wa nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Jasmin Sudi amewaomba wanachama wamchague ili aendeleze soka na kurudisha heshima ya mwanamke iliyopotea katika klabu hiyo.
Akizungumza na mwandishi wetu hili Dar es Salaam jana, Jasmin alisema jambo la kwanza atakalofanya ni kurudisha nguvu ya umoja wa wanawake wa Simba kwa kufanya nao kazi kwa karibu.
“Umoja wa wanawake ni muhimu katika klabu yetu kwani ni nguzo muhimu katika maendeleo ya Simba, lakini kwa siku za karibuni kundi hili limekuwa nyuma,” alisema.
Mgombe huyo alijinadi kuwa atalinda katiba ya Simba na kudumisha uhusiano mzuri baina ya matawi na wanachama wote wa klabuni hapo.
Alisema kwa kipindi cha miaka saba aliyofanya kazi kama katibu muhtasi wa klabu hiyo, amejifunza mengi na atakuwa mshauri mzuri kwa rais ajaye iwapo atachaguliwa kuwa mjumbe katika Kamati ya Utendaji, huku mkazo wake ukiwa katika soka.
Jasmin, ambaye ni mke wa beki wa zamani wa Simba, Victor Costa alibainisha kuwa maneno bila vitendo katika klabu yoyote ya soka, ni kujidanganya kwani mwisho wa siku soka linatakiwa lionekane.
“Simba kama klabu haiwezi kuwa imara bila kuhakikisha mpira unachezwa kwa kiwango cha juu uwanjani, hivyo ili kuhakikisha hilo linatimia ni vema kuchagua viongozi wa mpira na si wa maneno.
“Chagueni viongozi wapenda mpira, msichague wapenda ofisi na majigambo. Wapenzi na wadau wa soka hawataki maneno wanataka mpira siyo tu kuwapo bali kuonekana unachezwa kwa kiwango na hadhi ya timu yenye miaka mingi kama Simba,” alisema.
Jasmin aliongeza kuwa wakati wa kucheza soka la kelele na fitina umekwisha kutokana na kuwapo kwa upinzani wa kweli kwenye soka, hivyo wanachama wanapofanya uchaguzi walitilie maanani suala hil

Mdhamini wa Suarez amkana


Mchezaji wa Italy Chiellini na Luis Suarez
Mshambuliaji wa timu ya Uruguay Luis Suarez amempoteza mmoja wa wadhamini wake baada ya kupigwa marufuku kwa kumng'ata mchezaji wa Italy Giorgio Chiellini.
Kampuni ya kamari ya mtandaoni 888 poker imesema ''imeamua kusitisha mkataba wake na mchezaji huo mara moja''.
''Kila mtu anajua ni nini kilichomfanya Luis.
Walitaka aondolewe katika michuano ya kombe la dunia.Na kweli walifanikiwa.
''Walimuondoa katika mechi hizo kama mbwa'' alisema Lila Piris Da Rosa bibiye Suarez.
''Mchezaji huyo wa miaka 27 anayeichezea kilabu ya Liverpool alipigwa marufuku ya miezi minne na shirikisho la soka duniani FIFA baada ya kupatikana na hatia ya kumng'ata Chiellini katika mechi ya kombe la dunia.
"
Suarez hawezi kuchezea kilabu yoyote ama taifa lake hadi mwisho wa mwezi Oktoba.
kamari
Atakosa kushiriki katika mechi zilizosalia katika kombe la dunia nchini Brazil.
Uruguay itacheza na Colombia katika mechi za kumi na sita bora siku ya jumamosi baada ya kufuzu katika kundi la 'Da' nyuma ya Costa Rica.
Suarez alijiunga na kampuni ya 888poker kama mjumbe wake duniani siku chache kabla ya kuanza kwa michuano ya kombe la dunia na kutoa baadhi ya kanda za video za shajara ya mtandao wake ikiwemo moja ya bao lake wakati wa ushindi wa taifa lake dhidi ya Uingereza.

Wagonjwa wa Ebola watoroka hospitalini

Watu zaidi ya miatano tayari wamefariki kutokana na ugonjwa huo katika kanda ya Afrika Magharibi
Serikali ya Sierra Leone imeonya kuwa ni hatia kumpa hifadhi mtu yeyote aliyeambukizwa virusi vya Ebola.
Hii ni baada ya taarifa kuwa baadhi ya wagonjwa wametoroka hospitalini na kujificha.
Kwa mujibu wa wizara ya afya nchini humo, baadhi ya wagonjwa wa homa hiyo kali wametoroka hospitalini katika wilaya ya Kenema, kitovu cha mlipuko wa ugonjwa huo.
Shirika la afya duniani, WHO, limetoa wito wa hatua za haraka kuchukuliwa kudhibiti homa hiyo katika kanda ya Afrika Magharibi ambapo hadi sasa wagonjwa 400 wamefariki.
Mlipuko wa sasa wa ugonjwa huo ndio mkubwa zaidi kushuhudiwa hasa kwa kuwa umesabaisha vifo vingi na kuenea zaidi katika nchi nyinginezo za kanda hiyo.
Visa zaidi ya 600 vya ugonjwa huo vimeripotiwa nhini Guinea ambako ulianza miezi minne iliyopita na katika mataifa jirani ya Sierra Leone na Liberia.
Takriban asilimia 60 ya watu walioambukizwa ugonjwa huo wamefariki.
Shirika la afya duniani linasema kuwa watu 46 wako katika hali mahututi kati ya 176 walioambukizwa ugonjwa huo.
WHO limewatuma wataalamu 150 wa ugonjwa huo katika kanda ya Afrika Magharibi kuzuia kuenea kwa homa hiyo kali
Hadi kufikia sasa hakuna tiba inayojulikana ya ugonjwa huo na shirika la WHO limetuma wataalamu 150 wa magojwa kwenda katika kanda ya Afrika Magharibi kujaribu kupunguza kasi ya kuenea kwa ugonjwa huo.
Mmoja wa madaktari wanaosaidia katika juhudi za kupambana na ugonjwa huo alisema kuwa baadhi ya watu wamewapuuza katika juhudi zao za kuwahamasisha umma kuhusu homa hiyo hatari.
Alisema watu wamekuwa wagumu wa kuelewa na pia hawataki kuelimishwa wakiona kama ugonjwa huo sio tisho.
WHO limetahadharisha mataifa ya Ivory Coast, Mali, Senegal na Guinea Bissau kuwa macho kutokana na wasafiri wanaoingia nchini humo kwani huenda wakawa wameambukizwa homa hiyo.

Thursday, 26 June 2014

Rais wa Nigeria aahirisha Ziara kisa Bomu


Rais wa Nigeria Goodluck Johnathan
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ameahirisha ziara yake nchini Equitorial Guinea kufuatia shambulizi la bomu la siku ya Jumatano katika mji mkuu wa Abuja,kulingana na msemaji wake.
Usalama umeimarishwa katika mji huo kufuatia shambulizi hilo lililowauwa watu 21 na kuwajeruhi wengine 52.
Hatua ya Bwana Johnathan kurudi inafuatia shtuma kwamba ameshindwa kukabiliana na ghasia nchini humo.
Wapiganaji wa kundi la Boko haram wameimarisha mashambulizi yao nchini Nigeria.
Mnamo mwezi Aprili,wapiganaji hao waliwauwa zaidi ya watu 70 katika mlupuko wa bomu katika kituo kimoja cha basi viungani mwa mji wa Abuja.
Kundi hilo pia limekiri kutekeleza shambulizi la bomu lililotegwa ndani ya gari karibu na kituo cha mabasi katika kijiji cha Nyanya mnamo mwezi May,ambalo liliwauwa watu 19 na kuwajeruhi wengine 60.
kiongozi wa Boko Haram Abubakr Shekau

Hatahivyo kundi hilo halijatoa tamko lolote kuhusu mlipuko wa hivi karibuni.
Maafisa wa Polisi wanasema kuwa mshukiwa mmoja amekamatwa lakini hawajatoa maelezo yoyote kumhusu.
Msemaji wa rais Reuben Abati amesema kuwa Jonathan alipata habari kuhusu mlipuko huo wakati alipokuwa akiwasili katika hoteli yake katika mji wa Malabo nchini Equitorial Guinea alikoelekea kwa mkutano umoja wa afrika kulingana na gazeti la Premium Times nchini Nigeria.
Aliamua kurudi nchini Nigeria ili kukabiliana na tatizo hilo,alisema bwana Abati.
Mwandishi wa BBC Mansur Liman katika mji wa Abuja anasema kuwa vikosi vya usalama vimelitenga eneo hilo la mlipuko.
Maafisa wa polisi wameagiza kuongezwa kwa usalama pamoja na uchunguzi ndani na hata viungani mwa mji wa Abuja ili kuepuka mashambulizi zaidi,alisema.

Gavana wa akauni ya Lamuu Nchini Kenya Atiwa Mbaroni

Issa Timamy Gavana wa Kauti ya Lamu
Issa Timamy Gavana wa Kauti ya Lamu
Polisi nchini Kenya wamemkamata na kumzuia Gavana wa Kauti ya Lamu Issa Timamy kwa tuhma za kuhusishwa na mauaji ya zaidi ya watu 60 katika mji wa Mpeketoni na vitongoji vyake Juma lililopita.

Mkuu wa idaya ya makosa ya Jinai nchini humo Ndegwa Muhoro amethibitisha kukamatwa kwa Gavana huyo siku ya Jumatano na anatarajiwa kufikishwa Mahakamani siku ya Alhamisi.
Haijafahamika vema ni makosa gani Gavana huyo anatuhumiwa kuyafanya.
Juma hili watu wengine 11 waliuliwa na watu wasiojulikana katika Kaunti hiyo ya Lamu, juma moja tu baada ya mauaji ya zaidi ya watu sitini katika eneo la Mpeketoni.
Kundi la kigaidi la Al-Shabab nchini Somalia limekiri kutekeleza mauaji haya yote kutokana na jeshi la Kenya kuwa Somalia lakini serikali ya Kenya imesema mauaji hayo yalipangwa na kuchochewa kisiasa.
Rais Uhuru Kenyatta ameonya kuwa watu wote wanaoshukiwa kupanga na kutekeleza mauaji hayo yaliyolenga jamii ya Kabila moja iliyohamia katika eneo hiyo watachukuliwa hatua za kisheria.

Watu waliopoteza maisha Mpeketoni
Reuters
Upinzani nchini Kenya umekuwa ukiishinikiza wakuu wa usalama nchini humo kujiuzulu kwa kushindwa kuwalinda wakenya na kuwahakikishia usalama wao katika siku za hivi karibuni.
Inspekta wa Polisi David Kimaiyo alinukuliwa juma hili akisema hawezi kujiuzulu kwa kile alichokisema kuwa mauaji hayo yangezuiliwa kama sio kupangwa na kochechewa kisiasa.
Maeneo mengi ya Pwani nchini Kenya yamekuwa yakishuhudia mzozo wa ardhi kutokana na wenyeji wa eneo hilo kudai kuwa ardhi yao imenyakuliwa na wageni.

Benki ya Equity iliyochomwa moto katika mji wa Mpeketoni
Kuzorota kwa usalama Pwani ya Kenya tangu mashambulizi ya kigaidi ya Al Shabab yalipoanza nchini humo umesababisha nchi ya Uingereza kufunga Ubalozi wake mdogo mjini Mombasa na kuwawaomba raia wake kutozuru Pwani ya Kenya.
Mataifa mengine ambayo pia yamewarai raia wake kuwa makini wanapozuru Pwani ya Kenya ni pamoja na Ufaransa na Marekani.

Ghana yawafukuza Boateng na Muntari kwenye kikosi chao

Boateng na Muntari
Wachezaji wa kikosi cha timu ya taifa ya Ghana Sulley Muntari na Kevin Prince Boateng wamefukuzwa katika timu hiyo kwa ukosefu wa nidhamu.
Taarifa kutoka mtandao wa shirikisho la soka nchini humo imesema kuwa wawili hao wametimuliwa mara moja.
Boateng anayechezea kilabu ya Schalke 04 amefukuzwa kwa kutoa matamshi machafu yaliomlenga mkufunzi wa timu hiyo Kwesi Appiah wakati timu hiyo ilipokuwa katika mazoezi katika eneo la Maceio.
Naye mchezaji wa AC Milan Sulley Muntari ameadhibiwa kwa kumshambulia afisa mmoja wa kamati kuu ya timu hiyo
Shirikisho la soka nchini Ghana limeongezea kwamba kisa kinachomuhusu Muntari kilitokea siku ya jumanne na kumtaja Moses Armah,mwanachama wa usimamizi wa timu hiyo kama mtu aliyeshambuliwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29.
Wakati huohuo Boateng amedaiwa kutojali matamshi aliyoyatoa.Habari hizo zinajiri siku moja baada ya serikali ya Ghana kutuma dola millioni 3 nchini Brazil ili kuwalipa wachezaji wa timu hiyo nchini Brazil fedha zao za kushiriki katika michuano ya kombe la dunia.
Timu hiyo inayojulikana kama Black Stars ilikuwa imetishia kususia mechi kati yake na Ureno iwapo haitapewa fedha hizo swala lililoilazimu serikali kuingilia kati.
Ghana ina nafasi ya kufuzu katika michuano ya mchujo iwapo itaishinda Ureno na iwapo mshindi wa kundi G atakuwa Ujerumani.

Australia yatangaza eneo jipya la kuisaka ndege ya Malaysia

Ndege ya Malaysia ikiitafuta meli iliyoweka
Ndege ya Malaysia ikiitafuta meli iliyoweka

Serikali ya Australia imetangaza eneo jipya la kuitafuta ndege ya abiria ya Malaysia iliyotoweka na zaidi ya abiria 200 mwezi Machi mwaka huu.

Naibu Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Warren Truss amesema baada ya wataalam kuthathmini upya ni wapi ndege hiyo inawezakuwa iliangukia, eneo hilo jipya ni Kilomita 1,800 Pwani Magharibi wa Australia.
Ndege hiyo ya abiria MH370 ilitoweka ghafla ikielekea jijini Beijing nchini China ikitokea jijini Kuala Lumpur nchini Malaysia ikiwa na abiria 239 wengi wao wakiwa raia wa China.
Wataalam wanasema kuwa baada ya uchunguzi wao wamebaini kuwa ndege hiyo ilikuwa haindeshwi na rubani ilipozama.
Ripoti ya serikali ya Australia yenye ukurasa 64 imependekeza kuwa utafutaji huo ufanyika katika eneo la Kilomita 60,000 mraba.
Meli maalum ya Marekani ikiitafuta ndege ya Malaysia
Mwezi Aprili, Mataifa ya Magharibi yakiongozwa na Marekani yalituma meli maalum za majini kujaribu kuitafuta ndege hiyo sakafuni mwa bahari bila mafanikio.

Utafutaji wa ndege hii ndio ghali zaidi katika historia ya utafutaji wa ndege ya abiria iliyopotea katika mazingira ya kutatanisha. Familia za abiria waliotoweka baada ya kupotea kwa ndege hiyo wanasema wameghabishwa na kutopatikana kwa mabaki ya ndege hiyo ambayo hadi sasa haijulikani ilipo.

Suarez nje kombe la Dunia kwa Kumng'ata Giorgio

Suareza alisema awali kuwa baadhi ya matukio yanayotokea uwanjani hayapaswi kugeuzwa kashfa
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uruguay Luis Suarez amefungiwa mechi tisa na shirikisho la kandanda duniani Fifa baada ya kupatikana na hatia ya kumuuma mlinzi wa timu ya Italia Giorgio Chiellini kwenye mechi yao ya kombe la dunia nchni Brazil.
Suarez pia amefungiwa kutojihusisha na shughuli yoyote ya kandanda kwa miezi minne na kutozwa faini ya dola elfu mia moja.
Kutokana na adhabu hiyo Suarez sasa hatashiriki tena kwenye mechi zilizosalia za kombe la dunia.

Mlipuko waua 12 na kujeruhi 50 Nigeria

Moto ukiteketea kulikolipuka bomu nje ya kituo cha biashara Abuja, Nigeria.
Kumetokea shambulizi la bomu mbele ya soko lenye shughuli nyingi katika mji mkuu wa Nigeria Abuja na kuwauwa zaidi ya watu 21.
Taswira ya majonzi na kilio ilitanda katika mji wa Abuja, mamia ya watu waliokuwa wakinunua bidhaa katika soko hilo wakijikuta wakivuja damu kutokana na majeraha ya mlipuko huo na wengine kuishia mauti.
Bomu hilo lililipuka mbele ya kituo kikubwa cha biashara, kinachotembelewa na watu wengi.
Walioshuhudia walisema sehemu za miili ya wanadamu zilitapakaa kila mahali sakafuni.
Magari yalichomeka kabisa na vioo katika madirisha ya nyumba zilizokuwa karibu kuvunjika vyote. Watu waliokuwa na hofu walielekea kwenye mahospitali yaliyo karibu ambapo walishuhudia magari ya wagonjwa yakisongamana kila mahali yakiwaleta wagonjwa na miili ya waliokufa.
John Tobi Wojioa aliwasili mahali hapo muda mfupi baadaye akimtafuta jamaa wake. Alitaja alichoona kama mafuriko ya damu:
"Kulikuwepo magari ya wagonjwa wa shirika la FRCS (federal Road Safery Corps) na ya mashirika mengine yaliyokuwa yakiingia na kuondoka yakibeba miili ya waathirika. Kwenye barabara alama za damu za nyayo za wanadamu zilionekana kila mahali," alisema Bwana Wojioa.
Bahati kwa Bwana Wojioa ni kuwa jamaa wake baadaye alipatikana akiwa hai huku akiendelea kutulia kutokana na mlipuko huo.
Hii ni mara ya tatu kwa mji mkuu kulengwa na milipuko tangu Aprili. Kundi la Waismalu waenye itikadi kali la Boko Haramu lilidai kuhusika katika milipuko mbili ya awali ambako zaidi ya watu 90 walifariki.
Milipuko hiyo ilitokea kando mwa jiji lakini huu wa sasa umetokea katikati mwa jiji katika Wilaya ya Wuse 2 na hofu yake itatanda katika mji wote.
Kwa mara nyingine tena Boko Haram watashukiwa kuhusika katika mlipuko huu. Kundi hilo limelipua miji kadhaa nchini Nigeria huku likiendesha kampeni yake ya kuwashambulia raia katika maeneo ya mashambani hasa Kaskazini Mashariki mwa taifa hilo.
Mnamo Jumanne watu waliokuwa wakitoroka vijiji katika jimbo la Borno walisema kuwa makumi ya wanawake na watoto walikuwa wametekwa nyara.
Lakini Serikali kwa upande wake ikasema kuwa hakuna ushahidi kuwa utekaji nyara ulitendeka.
Serikali ilisema vivyo hivyo wakati zaidi ya wasichana wanafunzi zaidi ya 200 walitekwa nyara na Boko Haram mnamo Aprili.
Wachunguzi wengi wanasema kuwa kwa kukanusha kuwa kuna utovu wa usalama nchini Nigeria, Serikali imechanganyikiwa kwa sababu milipuko ya mabomu ya mara kwa mara ni ushahidi tosha kuwa ukosefu wa usalama ndio ukweli wa mambo nchini.

Warema na kafulila washikana mashati bungeni

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema (kushoto) akizuliwa na Mawaziri na Manaibu Waziri kutomfuata Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila baada ya kupandwa na hasira kufuatia mbunge huyo kumtuhumu kwa kumuita mwizi kwenye ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma jana

Kama siyo kuzuiwa na mawaziri, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema jana angezua tafrani bungeni kutokana na kitendo chake cha kutaka kumpiga Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila.
Sakata hilo lilitokea jana asubuhi baada ya Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu kuahirisha kikao cha Bunge hadi jioni, ikiwa ni muda mfupi baada ya Werema na Kafulila kurushiana maneno bungeni. Jaji Werema alichukia baada ya Kafulila kumwita mwizi, akijibu mapigo baada ya mbunge huyo kuitwa tumbili na mwanasheria huyo.
Waliomzuia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Simbachawene na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Abdulla Juma Saadallah.
Mawaziri hao walimsindikiza Werema hadi nje ya Ukumbi wa Bunge na kutoweka.
Ilivyokuwa
Hali ilianza kuchafuka wakati Jaji Werema alipokuwa akijibu mwongozo uliombwa na Kafulila kuhusu fedha za akaunti ya Escrow.
Katika mwongozo huo, Kafulila alisema Wizara ya Nishati na Madini kupitia Waziri wake, Profesa Sospeter Muhongo alizungumza uongo mara mbili bungeni kuhusiana na fedha za akaunti ya Escrow.
“Alisema uongo mbele ya Waziri Mkuu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika maeneo mawili, kwamba uamuzi wa kutoa fedha za Escrow kwa IPTL ulikuwa wa Mahakama na Serikali isingeweza kwenda kinyume...” alisema.
Alisema katika hukumu hiyo ya Septemba mwaka jana, hakuna mstari hata mmoja unaosema kuwa fedha za Escrow wapewe Kampuni ya IPTL.
“Profesa Muhongo aliliambia Bunge kuwa Serikali ililipa fedha hizo ili kuondokana na kesi hiyo lakini ninazo nyaraka za Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kuteua kampuni mbili za uwakili kwenda kuiwakilisha katika kesi nchini Uingereza,” alisema Kafulila.
Alisema kwamba aliomba mwongozo sababu huo umekuwa mwendelezo wa kuzungumza uongo bungeni... “Naibu Waziri (Nishati na Madini - Stephen Masele), alizungumza uongo bungeni tukaambiwa kuwa wamekutana katika sherehe za kuzaliwa yakaisha, haiwezekani, Bunge ni sehemu ya kuisimamia Serikali.
“Haiwezekani Bunge ling’olewe meno liwe ni chombo ambacho mtu anaweza kuzungumza uongo bila kuchukuliwa hatua kwenye jambo hili ambalo linaligharimu taifa mabilioni ya fedha.”
Baada ya madai hayo, Jaji Werema alisimama na kusema: “Bunge hili liliamua mambo mawili, kwanza kulikuwa suala la rushwa na CAG apewe kazi ya kuchunguza na kutoa taarifa bungeni. La pili kuna watu walitoa vipeperushi humu bungeni, miongoni mwao ni huyu anayetoa maneno machafu (Kafulila),” alisema Werema na kumfanya John Mnyika (Mbunge wa Ubungo-Chadema), kuomba mwongozo uliokataliwa na Mwenyekiti Zungu.
Hata hivyo, Mnyika na Kafulila waliendelea kuomba mwongozo, lakini Zungu aliwataka wamsikilize Jaji Werema kwa sababu naye alimsikiliza Kafulila. Werema aliendelea: “Suala la Escrow ni suala linalotokana na wanahisa wawili ambao ni IPTL na Mechmar… Pesa ya Serikali haikai kwenye Escrow.”
Hata hivyo, alikatishwa na kelele za Mnyika ambaye alitaka mwenyekiti kumpa nafasi ya kutoa taarifa.
“Sasa kama unataka kuleta mambo ya nje ndani ya Bunge ningojee pale nje,” Jaji Werema alisema wakati wabunge hao walipokuwa waking’ang’ania kutoa taarifa.
Alisema ugomvi huo ulitokana na wanahisa wawili hao kila mmoja akitaka IPTL ifilisiwe ili waachane. Alisema Serikali iliingia katika mgogoro huo kwa sababu ya mikataba ya udhamini na kwamba wakati wanagombana iliamua kufungua akaunti ya Escrow.
Hata hivyo, kuliibuka maneno tena kutoka upande wa Kafulila na Jaji Werema alitaka kusikilizwa hata kama yeye ni mtuhumiwa katika suala hilo.
“… Wanyankole wanasema tumbili hawezi kuamua masuala ya misituni… sikiliza tumbili, sikiliza ‘please’ (tafadhali),” alisema Werema.
Sentensi hiyo iliamsha kelele kutoka upinzani na Kafulila alisikika akimwita Werema mwizi.
Hata hivyo, Zungu alizuia vurumai hizo kwa kumtaka Jaji Werema kukaa na kisha kuwataka wabunge hao wawili kupeleka ushahidi wao Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (Takukuru).
Mara tu baada ya Zungu kuahirisha Bunge, Jaji Werema alisimama na kumfuata Kafulila lakini kabla hajamfikia, mawaziri hao walimzuia na kumsindikiza hadi nje.
Baadaye, Kafulila na Mnyika waliitisha mkutano na waandishi wakitaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda afute uongo huo bungeni ndani ya siku mbili na akishindwa, watakusanya sahihi za wabunge kumuondoa katika nafasi hiyo.Alipohojiwa kama ni vyema kwa Wassira alisema walimsihi Werema kuachana na Kafulila na kuendelea na shughuli zake.

Al shabaab Washambulia tena hotel


Wanajeshi wa Amisom nchini Somalia
Taarifa kutoka Somalia zinasema kwamba kumekuwa na makabiliano makali milipuko na milio ya risasi ikisikika katika eneo la hoteli moja inayotumika kama makao makuu ya vikosi vya Afrika vya kulinda amani.
Walioshuhudia shambulizi hilo wanasema hoteli hiyo iliyopo katika mji wa Bulo- burde, umeshambuliwa na wanamgambo wa Al -shabaab.
Hoteli hiyo inayotumiwa na wanajeshi wa Muungano wa Afrika AMISOM,pamoja na jeshi la Somalia katika eneo la Buuloburde, kati kati mwa Somalia ililengwa kwa mashambulizi na wapiganaji wa Al Shabaab.
Kundi hilo limekiri kufanya mashambulizi hayo, na kuongeza kwamba wamewaua angalau wanajeshi sita wa Amisom.
Msemaji wa Amisom alisema kuwa wanajeshi wake watatu wameuawa katika shambulizi hilo.
Wapiganaji wawili waliokuwa wamevalia magwanda ya kijeshi,walivamia hoteli hiyo na kuanza kuwapiga risasi wanajeshi. Walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa walisikia milio ya risasi kwa muda wa saa moja na nusu kabla ya wanajeshi hao kuwaua washambuliaji.
AMISON ilidhibiti eneo la Buuloburde mwezi Machi, lakini mji huo unasema kuwa al shabaab imezuia barabara zote kuelekea katika hoteli hiyo.
Wanajeshi wa Amisom, wanaweza tu kupata mahitaji yao kwa kutumia ndege.Wakazi wengi walitoeoka mjini humo na sasa wanaishi viungani wa mj wenyewe.

Wednesday, 25 June 2014

SHambulio jingine Kenya lashababisha Vifo vya watu 15

wakazi walokusanyika mbele ya majengo yaliyoharibiwa na shambulio la Jumapili huko  Mpeketoni, Kenya, June 16, 2014.
wakazi walokusanyika mbele ya majengo yaliyoharibiwa na shambulio la Jumapili huko Mpeketoni, Kenya, 
 
Washambuliaji wanaodhaniwa ni wanamgambo wa kundi la Al Shabab wamesababisha vifo vya karibu watu 15 katika shambulio jingine siku ya Jumatatu usiku  katika eneo la Poromoko katika mji wa Mpeketoni.

Kufuatana na waziri wa ndani Joseph Ole Lenku washambuliaji waliharibu kituo cha mawasiliano cha Safaricom kabla ya kuanza mashambulizi katika lengo la kuwazuia wakazi kuwasiliana na watu wa nje na kutoa onyo.

Tukio hilo linafuatia shambulio la Jumapili katika mji huo huo ambapo watu 48 waliuwawa na wakazi waliokuwa na hasira wanaripotiwa wamekusanyika kwa hasira wakimtaka waziri wa mambo ya ndani anayeaminika yungali katika mji huo kueleza nini kinachotokea.

Iraq yaomba msaada wa kijeshi toka marekan

Ndege ya Marekani isiyotumia rubani-Drone
Ndege ya Marekani isiyotumia rubani-Drone
Mkuu wa majeshi ya Marekani anasema Iraq imeiomba Marekani kusaidia kufanya mashambulizi ya anga ili kupambana na wanamgambo wa ki-Islam wa ki- sunni ambao wamechukua udhibiti wa miji muhimu ya kaskazini na wanaitishia kuishambulia Baghdad.

Mwenyekiti wa baraza la wakuu wa majeshi, Jenerali Martin Dempesy, ali-iambia kamati ndogo ya baraza la seneti la Marekani hapo jumatano kwamba serikali ya Iraq imeshindwa kuwalinda wananchi wake na amesikitishwa sana na jambo hilo.

Naye waziri wa ulinzi wa Marekani, Chuck Hagel alisema viongozi wa kishia nchini Iraq, hawajawahi kutekeleza jukumu lao la  kuunda serikali ya umoja wa kitaifa pamoja na wasunni na wakurdi.

Wakati huo huo, akisafiri kuelekea Colombia, Makamu Rais wa Marekani, Joe Biden alizungumza kwa njia ya simu na Waziri Mkuu wa Iraq, Nouri al-Maliki pamoja na viongozi wa kisuni na wa kikurdi. Alisisitiza juu ya umuhimu wa serikali ya umoja nchini Iraq  ambayo itaweza kukabiliana na kitisho kinachosababishwa na  wanamgambo, kwa wa-Iraq wote

Helikopta ya shambuliwa yaua 9

Helikopta sawa na ile iliyodunguliwa Ukraine na kuwaua watu 9.
Maafisa wa wizara ya ulinzi nchini Ukraine wamesema kuwa waasi wanaotaka kujitenga ambao wanaiunga mkono Urusi wamelipua ndege iliyokuwa imewabeba wanajeshi wa serikali na kuwauwa watu tisa.
Shambulio hilo lilifanywa karibu na mji wa Sloviansk unaodhibitiwa na waasi mashariki mwa taifa hilo.
Kulingana na maafisa wa Ukraine, helikopta hiyo ilipigwa risasi nje ya makao makuu ya Sloviansk.
Wanajeshi saba wa Ukraine ni miongoni mwa watu waliofariki katika tukio hilo.
Kudunguliwa kwa helikopta hiyo kumetokea muda mufpi baada ya Serikali na upande wa kundi linalotaka kujitenga kutoka kwa Ukraine linaloungwa mkono na Urusi kutangaza usitishaji wa mapigano.
Mnamo Jumanne Rais wa Urusi, Vladimir Putin, alitoa wito kwa Wabunge kubadilisha upigaji kura walioufanya Machi, uliomruhusu yeye kuwa na mamlaka ya kuingilia kijeshi maswala ya Ukraine.
Serikali ya Ukraine na mataifa ya Magharibi wanasema kuwa Urusi inawaruhusu wapiganaji na silaha kuingia Ukraine, hatua ambayo inachochea uasi unaoendelea nchini humo.
Lakini kiongozi wa eneo linalopiganiwa wakati huu linalotaka kujitenga lililojitangaza kama "jamhuri ya watu wa Donetsk", Alexander Borodai amesema kuwa kwa maoni yake haoni maana yo yote ya kusitisha mapigano.
"Nasema rasmi sasa kuwa hakujakuwepo na usitishaji mapigano na ukichunguza kwa makini kinachoendelea hakutakuwepo na usitishaji huo wa mapigano....kwa ujumla, kilichosalia kwetu sisi ni kuendelea kupigana," Alexander Borodai alisema.
Wakati huohuo Rais wa Urusi, Vladmir Putin, amesema kuwa haitoshi kwa Ukraine kutangaza siku saba za usitishwaji wa mapigano kati yake na waasi Mashariki mwa Ukraine.
Alisema mashauriano mengine kambambe yanapaswa kuandaliwa ili kuwahakikishia wachache wanaozungumza lugha ya Kirusi wanaoishi nchini Ukraine haki zao za kimsingi.

Tuesday, 24 June 2014

Algeria yaandika historia, yaifunga Korea 4-2

Algeria yaandika historia, yaifunga Korea 4-2Algeria imebadili historia na kuwa timu ya kwanza kutoka barani Afrika kushinda magoli manne katika fainali za kombe la dunia. Algeria iliifunga Korea Kusini jumla ya magoli 4-2.

Ilichukua dakika 26 tu kwa Algeria kupata goli lake la kwanza kupitia kwa Slimani kabla ya Halliche kutia goli la pili kimyani dakika mbili mbele. Haikuchukua muda mrefu zaidi kabla ya kupata goli la tatu katika dakika ya 38.
Kipindi cha pili kilikuwa na mikikimikiki mingi zaidi. Korea walijaribu kupunguza magoli na kupata goli la kwanza katika dakika ya 50. Hata hivyo Algeria walizidisha wimbi la magoli kwa kufunga goli katika dakika ya 62. Dakika ya 72 Korea walipata goli la pili na la mwisho.

Majambazi waua sista na kupora

  Wananchi wakiangalia sehemu ambayo majambazi walimpiga risasi Sista Clencensia Kapuli Ubungo, Riverside, Dar es Salaam jana.

 Majambazi wamemuua kwa risasi Sista wa Kanisa Katoliki Clencensia Kapuli (50) na kupora kiasi kikubwa cha fedha ambacho hakijajulikana.
Pia, katika tukio hilo lililotokea jana saa nane mchana eneo la Riverside, Ubungo, Dar es Salaam, dereva aliyekuwa akimwendesha Sista Kapuli, Patrick Mwarabu alikatwa kidole gumba kwa risasi.
Sista Kapuli wa Shirika la Mtakatifu Maria wa Parokia ya Mwenyeheri Anwarite, Makoka Jijini Dar es Salaam alikuwa mhasibu wa parokia hiyo ambayo inamiliki Shule ya Sekondari Mwenyeheri Anwarite na Chuo cha Ufundi Stadi Makoka.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura aliyefika katika Kituo cha Polisi Urafiki kufuatilia tukio hilo alisema Sista Kapuli na sista mwenzake wakiwa katika gari aina ya Toyota Hilux, walikuwa wakitoka Benki ya CRDB, Tawi la Mlimani City kuchukua fedha na walipita Riverside ndipo walipopatwa na mkasa huo.
“Bado hatujajua ni kiasi gani cha fedha kimechukuliwa kwa kuwa Sista Kapuli ndiye alikuwa mhasibu na ndiye aliyekwenda kuchukua fedha hizo, subirini tutakapokwenda benki kuuliza ni kiasi gani cha fedha alichukua na tutawajuza,” alisema Wambura.
Kamanda huyo alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ukisubiri taratibu za mazishi.
Shuhuda wa tukio hilo, Gadi Kinyamagolo alisema masista hao walikwenda Riverside kununua mchele katika moja ya maduka ya jumla.
“Mara baada ya kumaliza kununua mchele kama kilo 10 hivi walipanda katika gari wakiwa wawili na kabla ya kuondoka zilifika pikipiki mbili zikiwa na watu wanne, zikasimamisha gari hilo huku mmoja akiwa amevalia kininja na mwingine aliyevaa kawaida, wote wakiwa na silaha. Wengine wawili walibaki kwenye pikipiki.
“Kisha nikaona wanapasua kioo cha nyuma ambapo kulikuwa na sista mmoja na mwingine alikuwa mbele, wote wakiwa na mikoba ambayo majambazi hao waliiomba,” alisema Kinyamagoro na kuongeza:
“Walianza kuwaambia tupe mikoba huku majambazi hao mmoja akiwa amesimama upande wa dereva na mwingine upande wa pili wa gari alipokuwa sista aliyeuawa lakini masista wale hawakutoa mikoba hiyo.”
Kinyamagoro alisema: “Baada ya mabishano, sista aliyekuwa nyuma alifungua mlango na kukimbilia katika duka walilonunua mchele na yule aliyekuwa mbele alipofungua mlango akitaka kukimbia alipigwa risasi shingoni na kutokea upande wa pili na kuanguka nje ya gari.
“Baada ya tukio hilo majambazi hayo yalichukua mikoba miwili na kuondoka nayo. Kwa kuwa mimi nilikuwa karibu nililala chini na eneo hili lilikuwa kimya, watu walikimbia na wengine tulilala tukaacha wafanye kazi yao.”
Shahidi mwingine, Saidi Juma alisema: “Wakati majambazi hao wakiondoka palikuwa na watu wawili waliovalia sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakipita eneo hilo, waliulizwa na majambazi wanafanya nini huku wakiwa wameonyeshwa bunduki. Walinyoosha mikono juu na kuachwa, kisha majambazi wakapanda pikipiki zao na kutokomea.
“Wakati majambazi wakiondoka watu hao waliruka na kulala mtaroni kukwepa kupigwa risasi. Majambazi walipofika hapo mbele (mbele kidogo ya eneo la tukio), walimpiga risasi muuza machungwa na kumjeruhi begani.”

Barabara ya Serengeti yazuiwa kujengwa

Kufuatia Mahakama ya Afrika Mashariki kuizuia serikali ya Tanzania kujenga barabara ya lami kupitia hifadhi ya Serengeti, wakazi wa maeneo hayo wamepinga uamuzi huo na kudai kuwa mradi wa barabara hiyo ni wa lazima na manufaa kwao.
Ujenzi huo umezuiwa na mahakama kufuatia taasisi mbalimbali za nje ya Tanzania kuweka pingamizi kwa madai kuwa ujenzi huo utaathiri mazingira, maisha ya wanyamapori na bayoanuai ya hifadhi hiyo.
Wakipinga uamuzi huo wa mahakama, wakazi wa maeneo hayo ambako barabara hiyo ya lami inatarajiwa kupita wamesema mahakama hiyo ya Afrika mashariki, pengine imepelekewa mashtaka yasiyo sahihi, na kutolea maamuzi masuala yasiyo wahusu.
Onesmo Olengurumwa, Makamu mwenyekiti wa Umoja wa Watu wa Ngorongoro, anasema walichotaka wao ni kutengenezewa barabara ya lami, kwa ajili ya kuharakisha maendeleo katika maeneo yao.
Shughuli ya ujenzi wa barabara
''Hatukuwa na mpango wa kutengeneza barabara kubwa yenye kupita magari mengi kwa mwendo wa kasi, kama ilivyoelezwa kwenye maelezo yaliyotolewa mahakamani’’.
Tanzania haitaki kuingiliwa
Amesema Tanzania haiwezi kuingiliwa katika kutengeneza barabara za wananchi wake kwa ajili ya maendeleo yao.
Hukumu hiyo ilitolewa baada ya taasisi inayoshughulika na masuala ya wanyama ya (Africa Network For Animal Welfare) ya nchini Kenya kufungua kesi dhidi ya Serikali ya Tanzania.
Kesi hiyo inalenga kupinga ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa Kilomita 239, ikidai itaathiri mazingira, uhai wa wanyama na baioanuai katika hifadhi hiyo, ambaoo ujenzi wake utasababisha kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu.
Watalii Serengeti
Kufuatia uamuzi wa taasisi hiyo kuipeleka mahakamani serikali ya Tanzania mbunge wa Ngorongoro Kaika Saning'o Telele aliitupia lawama nchi jirani ya Kenya kwamba ina mbinu za kukwamisha mipango ya maendeleo ya nchi yake kwa maslahi yake.
''Ndugu zetu wa Kenya , kila wakati serikali yetu inapokuwa na jambo kubwa inataka kulifanya kwa ajili ya wananchi, wamekuwa wakija na hoja za mazingira na wanyamapori, kama vile sisi hatuelewi masuala hayo’’
Kwa mujibu wa serikali ya Tanzania, barabara hiyo ingepitia Mto wa Mbu-Engaruka-Loliondo-Kleins Gate-Serengeti-Mugumu-Nata na kuungana na ile ya Tarime-Musoma-Mwanza, hivyo kupunguza adha ya usafiri kwa wananchi wa maeneo hayo ambao baadhi hulazimika kupitia Nairobi nchini Kenya.

Monday, 23 June 2014

Mauaji mengine yatokea Kenya

Moja ya mashambulizi ya kigaidi yaliyowahi kutokea nchini Kenya na kusababisha maafa
Kuna taarifa kuwa watu ishirini wameuawa katika shambulio kwenye kijiji Mashariki Kaskazini mwa Kenya.mashuhuda wanasema watu wenye silaha walivamia kijiji cha Gunana katika County ya Wajir mapema siku ya jumapili.
Amesema mapigano yalizuka kutoka na mgogoro baina ya koo mbili za Degodia na Gare.
Ni mzozo wa mpaka baina ya koo hizo ambao wakuu wanautambua, lakini bado hawakuweza kuupatia ufumbuzi.
Aidha mwandishi wa shirika la utangazaji la uingereza  BBC wameongeza kuwa pamoja na kwamba kuliwahi kutokea mapigano mengine hapo awali lakini hayajawahi kusababisha vifo vya watu wengi kwa mara moja kama ilivyotokea siku ya jumapili.
Mauaji haya yanakuja wiki moja baada ya watu wapatao 60 kuuwawa katika mashambulizi mawili yaliyotokea eneo la Mpeketoni katika pwani ya Kenya lililodaiwa kufanywa na wapiganaji wa Al Shabaab .
Wapiganaji hao walivamia vijiji viwili karibu na mji wa Mpeketoni, na kufanya mashambulizi ambapo katika la kwanza lilisababisha mauaji ya wau 48 na baadae la pili liliua watu wapatao 20

Sunday, 22 June 2014

Waziri wa mambo ya nje Marekani Azuru Misri


Waziri wa maswala ya kigeni nchini marekani John Kerry
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani JohnKerry yupo mjini Cairo nchini Misri ili kukutana na rais mpya wa Misri Abdul Fatah Al Sisi.
Ni Mwanasisa wa hadhi ya juu kuzuru nchini Misri tangu kamanda huyo wa zamani wa jeshi kuchaguliwa kama rais baada ya kumpindua aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi.
Maafisa wa Marekani wanasema kuwa bwana Kerry yuko nchini humo kumtaka rais Al sisi kuwashirikisha watu wote katika siasa yake ikiwemo wanachama wa kundi la Muslim Brotherhhod lililopigwa marufuku.
Kerry pia anatarajiwa kuzungumzia kuhusu hukumu ya kifo iliotolewa dhidi ya wanachama wengi wa kundi hilo mbali na kutoa wito wa kuachiliwa kwa waandishi waliofungwa.
Waandishi walio katika ziara hiyo ya bwana kerry amesema kuwa Marekani iko tayari kuanzisha mazungumzo na rais huyo mpya ikiwa na matumaini kwamba mazungumzo hayo yataleta natija.

Malinzi abariki uchaguzi wa SIMBA SC bila Wambura

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) baada ya kupokea na kuzingatia maombi ya Simba (barua imeambatanishwa), na kwa kuzingatia Ibara ya 26 ya Kanuni za Uchaguzi za TFF toleo la 2013 limeiruhusu klabu hiyo kuendelea na mchakato wa uchaguzi wao uliopangwa kufanyika Juni 29 mwaka huu.

Taarifa ya TFF iliyotumwa leo imesema kwamba inawahimiza wanachama wa klabu ya Simba kuwa watulivu na wafanye uchaguzi wao kwa amani.
Ikumbukwe TFF ilisimamisha mchakato wa uchaguzi wa Simba SC hadi hapo klabu hiyo itakapounda Kamati ya Maadili ambayo itasikiliza masuala ya kimaadili kuelekea uchaguzi huo.

Malinzi alisema mwishoni mwa wiki kwamba Simba SC inatakiwa kuwa imekwishaunda Kamati ya Maadili hadi kufika Juni 30, mwaka huu, hatua ambayo alidai imefuatia TFF kupokea malalamiko mengi juu ya ukiukwaji wa maadili kwa baadhi ya wagombea na wanachama wa klabu hiyo.
Malinzi alisema kwamba baada ya kuundwa kwa Kamati hiyo Maadili itasikiliza malalamiko yote ya kimaadili yanayougubika mchakato wa udhaguzi huo, ambao ulipangwa kufanyika Juni 29, mwaka huu.
Aliagiza Kamati ya Utendaji ya Simba SC iliyopo madarakani chini ya Mwenyeiiti wake, Rage iendelea kuiongoza klabu hiyo hadi hapo mchakato wa uchaguzi utakapokamilika.    
Lakini mwanzoni mwa wiki, Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC ilimpinga Malinzi, ikisema TFF haina mamlaka ya kusimamisha uchaguzi huo na Jumanne, Rage akamuomba raisi huyo wa TFF aache mchakato wa zoezi hilo uendelee kwa manufaa ya Simba SC.
Juzi Kamati ya Rufani ya TFF iliitupilia mbali rufaa ya Michael Wambura kupinga kuenguliwa kugombea urais katika uchaguzi wa klabu ya Simba unaotarajiwa kufanyika baadaye mwezi huu.
Wambura aliwasilisha rufani yake mbele ya Kamati hiyo iliyokutana siku hoyo (Juni 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam chini ya Kaimu Mwenyekiti Wakili Mwita Waissaka kupinga uamuzi wa kumwengua katika kinyang’anyiro hicho uliofanywa na Kamati ya Uchaguzi ya Simba kwa kufanya kampeni kabla ya muda uliopangwa.
Baada ya kupitia vielelezo, kanuni na sheria, Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF imeridhika kuwa mrufani (Michael Wambura) alifanya kampeni kabla ya muda kinyume na Ibara ya 6(1)(a) na (g), Ibara ya 6(1)(l) pamoja na Ibara ya 14(3) ya Kanuni za Uchaguzi za TFF toleo la 2013.
Kwa mujibu wa ibara hizo, Kamati ya Uchaguzi ya Simba inayo mamlaka ya kumwengua (disqualify) mgombea anayefanya kampeni ama kukiuka maagizo halali ya Kamati ya Uchaguzi.
Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF imeziagiza kamati zote za uchaguzi za wanachama wa TFF kufuata kanuni za uchaguzi kama zilivyoainishwa katika Katiba zao ili kuepusha rufani za mara kwa mara.
Uamuzi wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF umezingatia Katiba ya TFF pamoja na kanuni zake, na pia Katiba ya Simba na kwa taarifa ya leo ya shirikisho hilo, Simba SC wanarudi rasmi kukimbizana na muda kuawahi uchaguzi wao.

Jose Mourinho asema England hawana cha kulaumu kwa kutolewa katika kombe la Dunia

England haina haja kusikia aibu yeyote kwa kutolewa mapema kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil kwa mujibu wa Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho.
England, wakicheza Kundi D la Fainali za Kombe la Dunia, walifungwa Mechi zao zote mbili za kwanza na Italy na Uruguay, zote kwa Bao 2-1 kila moja, na wamebakisha Mechi moja dhidi ya Costa Rica ambayo kwao ni kukamilisha Ratiba tu.
Mara ya mwisho kwa England kushindwa kuvuka hatua ya Makundi ni Mwaka 1958.
Lakini Mourinho amewapa moyo kwa kusema: “Sisikii vizuri kuiponda England kwa sababu hawastahili kusikia aibu kwa hili. Hawakuwa na Miungu ya Soka upande wao!”
Mourinho anaamini England walipewa kazi ngumu sana walipowekwa Kundi moja na Italy na Uruguay.
Kocha huyo kutoka Uremo alisema: “England hawakuwa na bahati. Imetokea Kundi lao lina Mabingwa wa Dunia Watatu ambao ni Uruguay, Italy na England. England walicheza vizuri, walishindana vizuri, hawakuziogopa Italy wala Uruguay!”
Jumanne Juni 24 England watacheza na Costa Rica ambayo tayari imetinga Raundi ya Pili ya Mtoano.
KOMBE LA DUNIA-Brazil 2014
MSIMAMO:

KUNDI D
TIMU P W D L F A GD PTS
Costa Rica 2 2 0 0 4 1 3 6
Italy 2 1 0 1 2 2 0 3
Uruguay 2 1 0 1 3 4 -1 3
England 2 0 0 2 2 3 -1 0