Tuesday, 6 May 2014

Shambulio la angani nchini Syria lasababisha vifo vya watu 15

Syria imekubwa na shambulio la bomu kutoka angani


Taarifa kutoka katika Baraza la Mapinduzi la Syria (SRGC) limebaini kuwa, ndege moja ya kikosi cha kivita ikiwa katika udhibiti wa wapiganaji wa upinzani ilishambulia  mji wa Idlib lililoko katika eneo la Armanaz kwa ''bomu ya vacuum''.
shambulio-la-angani-nchini-syria
Katika tukio hilo watoto 5 na watu 10 walipoteza maisha yao huku mamia ya watu wakijeruhiwa.
Katika taarifa kutoka Kamati ya Uratibu ya Syria (LCC) imebainika kuwa nyumba ziliporomoka na hasara kukadiriwa huku huduma nyingi za usafiri zikipoteza utendakazi wao.Vikosi vya ulinzi wa raia vilitumia huduma au vifaa vyao vya kazini ili kuondoa maiti na majeruhi waliofukiwa katika tukio hilo.
Taarifa ya LCC ilieleza kuwa raia walilazimika kutoroka wakati wa shambulizi la angani kutoka kwa vikosi hivyo vya utawala

No comments: