Idadi ya vifo vimeongezeka na kufikia 46 baada ya jengo moja kuunguzwa katika mji wa Kusini mwa Ukraine, Odessa.
Jengo la umoja liliunguzwa baada ya kuzuka mapigano baina ya makundi ya Kiukraine na makundi ya Kirusi na kusababisha watu 46 kupoteza maisha na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa.
Ukraine imetangaza siku mbili za maombolezo ishara ya kuwakumbuka waliopoteza maisha katika tukio hilo.
Wakati huohuo mivutano katika mji wa Mashariki ya Ukraine, Donetsk imefika katika kilele.
Kundi la Kirusi lilishikilia jengo hilo la ulinzi wa taifa.
Mamia ya kundi hilo walivunja madirisha na milango ya jengo hilo na kuchoma nyaraka zote pamoja na bendera ya Ukraine.
Kundi hilo tena likavamia makao makuu ya Kampuni inayomilikiwa na meya wa mji wa Donetsky, Sergey Taruta ambaye aliwekwa na uongozi wa Kiev.
Kundi hilo la Kirusi limesema kuwa halimtambui Taruta kama Gavana wa mji.
Katika upande mwingine, waziri wa mambo ya nje wa Ukraine ambaye alifanya maongezi na washirika wake, Marekani anaifanyia kazi hali hiyo ya sasa.
Lavrov ameitaka serikali ya Marekani kutia shinikizo kuzuia operesheni za majeshi ya Kiev huko Mashariki na Kusini mwa Ukraine.
Pia Lavrov ameomba kuongezeka kwa uwajibikaji wa jumuia katika ulinzi na ushirikiano Ulaya.
Wakati huohuo waangalizi 7 wa kimataifa wa kijeshi ambao ambao walikua wakifanya kazi yao huko mashariki ya Ukraine walipokamatwa wiki iliyopita, waliachiwa siku ya Mei 3.
No comments:
Post a Comment