Saturday, 10 May 2014

TBC tuko kibiashara zaidi

Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Utangazaji (TBC), Clement Mshana amesema kuwa wameamua kuonyesha mechi za fainali za Kombe la Dunia kupitia kituo cha televisheni cha TBC2 badala ya TBC1 ili waweze kuuza ving’amuzi vya StarTimes kwa madai kuwa wamewekeza fedha nyingi.
TBC1 na TBC2 zitaonyesha mechi zote 64 za fainali za Kombe la Dunia, lakini baadhi ya mechi hazitaonekana TBC1, ambayo hutumika kurusha matangazo yake kama huduma kwa wananchi kupitia ving’amuzi vya Continental, Digitech, Zuku, Ting na vingine.
Hata hivyo, Mshana alisema shirika lake, ambalo linategemea ruzuku zinazotokana na kodi ya wananchi, itatumia fursa hiyo kuuza ving’amuzi vya StarTimes, ambayo ni ya malipo.
“Sisi tunafanya biashara ya kuuza ving’amuzi vyetu vya Star Times. Hatuwezi kuwapa faida watu wengine... hii ni biashara na tumelipia. Msiniulize ni kiasi gani maana sitawambia kutokana na upinzani wa biashara uliopo.”
“Wale wenye ving’amuzi vya Star Times watapata huduma hii bure. Hawatalipia ingawa chaneli ya TBC2 ni ya kulipia, kipindi chote cha Kombe la Dunia wataipata chaneli hii bure na tutaonyesha mechi zote 64 na pia mechi hizo zitatangazwa na TBC FM.
“Na kwa wale ambao hawana king’amuzi cha StarTimes kuna baadhi ya mechi ambazo zinachezwa kwa muda mmoja watapata fursa kuona kwenye TBC1, ingawa si mechi zote ni

No comments: