Thursday 1 May 2014

Chelsea ya lazwa 3 1 Fainal zakutanisha Timu za jiji moja

article-2617143-1D7BEDE500000578-530_634x450KWA mara ya kwanza dunia itashuhudia fainali ya kwanza ya UEFA mei 24 mwaka huu mjini Lisbon, Ureno, itayozikutanisha timu mbili zinazotoka mji mmoja yaani Madrid.
Hii ni baada ya Atletico Madrid kufuzu fainali usiku huu kufuatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Chelsea kwenye uwanja wa Stamford Bridge.
Mechi ya kwanza nchini Hispania katika uwanja wa Vicente Calderon, timu hizi zilitoka suluhu, lakini leo Chelsea wameachia na kutolewa kwa wastani wa mabao 3-1 katika mechi zote mbili za nusu fainali.
Katika mchezo wa leo, Fernando Torres alitangulia kuifungia Chelsea dakika ya 36 kwa pasi ya Azpilicueta baada ya kazi nzuri ya Willian.
Dakika 8 baadaye, Adrian Lopez akaisawazishia Atletico kwa pasi ya Juanfran.
Diego Costa katika dakika ya 61 alifunga bao la pili kwa penalti iliyosababishwa na Samuel Eto`o.
article-2617143-1D7BCD8D00000578-458_634x415Wakati Chelsea wakihaha kusawazisha bao hilo, dakika ya 72, Arda Turan alipiga kidude cha tatu na jahazi la Chelsea kutota kabisa.
Mouringo katika dakika ya 54 alimtoa beki wake, Ashley Cole na nafasi yake kuchukuliwa na mshambuliaji, raia wa Cameroon, Samuel Eto`o ambaye alisababisha penati iliyowapoteza Chelsea.
Mabadiliko haya yaliwashitua wengi, lakini Mourinho ndiye kocha na anajua kwanini alifanya mabadiliko kama hayo kwenye mchezo muhimu kama huo.
Sasa Atletico watakutana na Real Madrid ambaojana waliwavua ubingwa Bayern Munich kwa kuwatandika mabao 4-0, jumulisha la Santiago Bernabeu ngoma inakuwa 5-0.
article-2617143-1D7BD5E700000578-98_634x420Baada ya mechi hiyo, Jose Mourinho amemsifu kipa wa Atletico Madrid, Thibaut Courtois kwa kufanya kazi nzuri ya kulinda lango lake.
“Mchezo kufikia muda fulani ulikuwa sawa sana, sana, sana , sana “. Mourinho ameuambia mtandao wa Sky sports.
“Kipindi cha kwanza kilikuwa chetu kuliko wao, lakini kumaliza 1-1 yalikuwa matokeo ya wazi. Na kipindi cha pili kiliamua kila kitu”.
“Dakika ambayo golikipa wa Atletico aliokoa kichwa cha John Terry nilidhani haitawezekana. Penati iliua mchezo. Sijui kama ni penati, nilikuwa mbali sana”.
“Ilikuwa dakika muhimu kwa Atletico baada ya kupata penati. Baada ya matokeo ya 2-1 dhidi ya Atletico nilijua sasa haiwezekani”.
“Na baada ya pale mchezo ukabaki kwa timu iliyokuwa na morali kwani walijua wana dakika 30 tu za kumaliza mchezo na wakaamua matokeo”. Amesema Mourinho.

No comments: