Magaidi wanawokusiwa kuwa wana Boko Harum wameteka nyara wasichana watatu pia.
Washukiwa wa ugaidi Boko Haram wameuwa zaidi ya wananchi 200 katika eneo la Gamboru Ngala ambapo ni mahala pa wakimbizi wa Nigeria na Cameroon, takriban kilometa 200 kutoka Maiduguri, mji mkuu wa mkoa wa Bono.
Seneta wa Bono aliitarifia Anadolu Agency kupitia kwa simu siku ya Jumatano kwamba zaidi ya watu mia 200 waliuwawa.
Aliongezea kwamba duru za maeneo hayo ziliiweka idadi hiyo kuwa 300.
"Magaidi hao walitekeleza janga hilo pasi pingamizi lolote," aliongezea.
Alizidishia kwamba magaidi hao waliwazengua maafisa wa usalama mpaka wakaacha kupiga doria.
"Maafisa wa usalama walipokea duru za uwongo kwamba magaidi wapo eneo karidi na ziwa Chad walakini walipofika walipatwa na habari za janga la mauwaji haya."
Maafisa wa usalama wa Nigeria wanajitahidi kuwapata wasichana waliotekwa nyara na magaidi wa Boko Haram mwezi uliopita.
Na'allah Ibrahim, mkaazi wa eneo la Gambro, aliripoti kwamba magaidi hao walikuwa wamevalia sari za kijeshi.
"Walitumia vifaa vya hali ya juu kama roketi na mabomu hatari." alielezea AA.
Ibrahim alitaarifu kwamba magaidi walichoma nyumba zote walizoziona na kufyatua risasi ovyo ovyo kana kwamba wapo vitani.
"Kwa mujibu wa Mola, sisi ni binadamu wasio sitahili haya, mbona jameni??" alilia huku akieleza.
Seneta pamoja na Ibrahim walitaarifu kwamba mashambulizi hayo yalitokea Jumatatu usiku.
-Wasichana zaidi watekwa nyara-
Wakati huo huo, watu waliojihami kwa binguki kukisiwa kuwa biko haram walivamia kijiji cha Wala Jumatatu nakuteka nyara wasichana zaidi.
No comments:
Post a Comment