Mancity yaweka hai matumaini ya ubingwa
Manchester
city wameweka matumaini ya kutwaa ubinga wa ligi hai baada ya
kuicharaza Everton 3-2 katika mchuano mgumu uliosakatwa ugani Goodison
Park.
Everton ilitangulia kufunga kupitia mchezaji Ross Barkeley katika dakika ya 11. Man City walisawazisha katika dakika ya 22 kupitia mshambuliaji matata Sergio Aguero. Edin Dzeko alipachika wavuni bao la pili na la tatu. Everton waliweza kupata bao la pili kupitia mchezaji Lukaku bali jitihada zao za kusawazisha hazikufua dafu.
Everton walitarajia kushinda na kujipa matumaini ya kufuzu kwa ligi ya mabingwa wa ulaya pamoja na kuwasaidia majirani wao Liverpool kunyakua ubingwa wa ligi ya Uingereza.
No comments:
Post a Comment