Msemaji wa makundi zinazounga mkono Urusi alisema waangalizi hawo waliachiliwa kama ishara ya nia njema .Inaripotiwa kuwa waangalizi hawo waliondoka Sloviansk, ambapo kazi ya jeshi la Kiukreni bado unaendelea, lakini hakuna taarifa zozote zinazotolewa kuhusiana na penye walichukuliwa.
Mwakilishi wa Urusi Vladimir Lukin ambaye alikuwa anafanya mashauriano juu ya kuachiliwa kwa waangalizi hawo wa kijeshi, aliwaambia waandishi wa habari kuwa watu wote 12 ambao walikuwa katika orodha yake wamekuwa huru.
Waangalizi wanane wa kijeshi, ambao walikuwa wametumwa katika Ukraine na Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya (OSCE) na maafisa watano wa kijeshi la Kiukren walikamatwa na makundi zinazounga mkono Urusi wiki iliyopita na kupelekwa Sloviansk.
Mwaangalizi wa Swedish aliachiliwa huru hapoa awali kutokana na matatizo ya kiafya. Timu hio ilihusisha maafisa wanne wa Ujerumani, Polish mmoja, Czech na afisa mmoja wa Kidenmark.
No comments:
Post a Comment