Bosi wa Chelsea Jose Mourinho anaamini Eden Hazard hayuko tayari kujitolea kwa ajili ya timu.
Jose
Mourinho amejibu mapigo kwa winga wake Eden Hazard aliyekosoa mbinu zake
za ufundishaji wa mpira kwa kueleza kuwa winga huyo wa Chelsea kwa
asilimia 100 hajitolei kwa ajili ya klabu yake.
Bosi
huyo wa Chelsea ameanza mkutano wake na waandishi wa habari mchana wa
leo kwa kumtetea Mbelgiji huyo kwa maneno aliyokaririwa na vyombo vya
habari kwa kufafanua kuwa maneno ya Hazard `yalibadilishwa`, lakini
Mourinho alihitimisha kwa kusema kuwa hakumfurahia winga huyo.
.
“Hakunikosoa. Ni kawaida kupata maoni kwa wachezaji kama yeye ili
kutatua matatizo kama tuliyokuwa nayo katika goli la kwanza dhidi ya
Atletico”
“Mechi
ya kwanza ya UEFA, Willian alicheza winga ya kushoto na kumsaidia sana
Cole. Eden ni mchezaji ambaye hana akili ya kumwangalia beki wake wa
kushoto”.
Hazard (kushoto) alikaririwa akisema Chelsea hawafundishwi soka la kisasa
Mourinho pia anaamini maneno ya Hazard juu ya mbinu zake za ufundishaji yamebadilishwa na vyombo vya habari
No comments:
Post a Comment