Martinez ameweza kuwatumia vizuri
wachezaji wake wa mkopo akiwa Goodison Park, Romelu Lukaku, Gerard
Deulofeu na Gareth Barry na wote wamekuwa katika kiwango cha kuvutia
katika klabu hiyo ya Merseyside.
Kocha huyo atamkosa Barry
jamamosi kwenye mchezo dhidi ya Manchester City kwasababu sheria ya
mkopo haimruhusu kucheza na klabu yake inayommiliki.
Kocha huyo wa zamani wa Wigan
Athletic amesema imefika wakati watu wa sheria za ligi kuu nchini
England waliangalie hilo, huku akionesha mfano jinsi Atletico Madrid
walivyomtumia Thibaut Courtois dhidi ya mwajiri wake wa kudumu, klabu ya
Chelsea kwenye mechi za nusu fainali za UEFA.
“Unapofikia makubaliano ya kumtoa mchezaji kwa mkopo, aruhusiwe kucheza”. Martinez alisema.
“Sioni kama ni haki kumnyima mchezaji haki ya kucheza na klabu yake aliyomwajiri”.
“Ni haki kufanya kama ilivyo
katika mashindano ya ulaya, kumuona mchezaji akicheza na timu yake
iliyomwajiri ni jambo zuri na nadhani itakuwa jambo la maana na baada ya
msimu ataangaliwa kiwango chake”.
“Sheria ya mkopo inahitaji mabadiliko ili kuendana na soka la kisasa. Ni mjadala mzuri na ni jambo la kuangaliwa kwa ndani”.
“Hatupaswi kuwa na sheria mbili
tofauti katika mashindano. Nadhani sheria za ligi ya ndani ziende
sambamba na sheria michuano ya ulaya”.
No comments:
Post a Comment