Monday, 5 May 2014

Tren yauwa watu 13 nchini India.

Duru za India zaripoti kwamba treni ilikosea mwendo kusini mwa India kiauwa watu 13 na kujeruhi mamia.
ajali-ya-gari-moshi-yauwa-watu-13-nchini-indi
Kilomita 110 kusini mwa Mumbai, gari moshi hilo lilikosea mwendo na kusababisha ajali hio. Waokowaji abiria walitumia misumeno kukata vyuma ili waweze kuwaokoa walioathirika. Kulingana na Shinde, magari ya nguvu yalitumiwa kuvuta na kutowanisha treni hio. Mzungumzaji wa shirika la reli la India bw. Anil Kumar Saxena alirepoti kwamba treni hiyo ilipokosea mwendo iligawanyika vipande viwili huku kimoja kikipenduka ilhali chengine kikibaki katika njia yake.
Usababishaji wa ajali hiyo bado haujajulikana. Maafisa wa reli wameagiza uchunguzi wa kina ufanywe upesi. Usafiri wa treni katika eneo hilo umepigwa marufuku kwa muda usiojulikana hadi ajali hilo itatuliwe na treni hiyo iondolewa njiani. Ajali za treni nchini India zimekuwa jambo la kawaida ilhali nchi hii ndio yenye idadi kuu wa treni na takriban wati milioni 20 hutumia usafiri huu kwa siku. Ajali nyingi hukusiwa kusababishwa namakosa ya kibinadamu au hali dohofisha ya treni.

No comments: