Sunday, 4 May 2014

Demba Ba aibua kesi Anfield

LIVERPOOL imeripotiwa kuanza kufanya uchunguzi juu ya madai kwamba straika wa Chelsea, Demba Ba alifanyiwa ubaguzi katika mchezo wa Ligi Kuu England uliofanyika kwenye Uwanja wa Anfield Jumapili iliyopita.
Ripoti hiyo inabainisha kwamba malalamiko hayo yaliletwa na kundi linalopinga ubaguzi la Kick It Out baada ya shabiki wa Liverpool kudaiwa kutoa kauli ambazo zilionekana kuwa ni za kibaguzi.
Ba, ambaye alisema yeye binafsi hakusikia ubaguzi huo, alifunga bao la kwanza wakati Chelsea walipoinyuka Liverpool mabao 2-0 na kuwatibulia kasi yao katika kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail, msemaji wa Liverpool alisema: “Tunatambua kuhusu malalamiko yaliyoletwa na Kick It Out na tupo kwenye uchunguzi wa jambo hilo.”

No comments: