Thursday, 8 May 2014

Maandamano Marekani Kusini.


Wananchi wa Argentina, Colombia na Haiti, japokuwa na sababu tofauti tofauti, walimiminika mitaani mwao kwa maandamano.

Katika mji wa Resistencia, Argentina mamia ya wafanyikazi wa umma pamoja na mawakilishi wa muingano ya wafanyikazi wa umma walikabiliana na polisi walipokuwa wakiandamana hadi majengo ya serikali.
Polisi walitumia risasi za mpira na gesi ya machozi ili kuwatawanyisha wanaharakati hao.
maandamano-marekani-kusini
baadhi ya waandamanaji
Nako Colombia, wanafunzi waligeuza mtaa wa Bogoti uwanja wa vita kwa kuuchoma moto kwa mujibu wa kuwauga wakulima katika mgomo wao. Polisi walilazimika kutumia nguvu kuepusha hasara zaidi.
Makundi ya pembezoni waliofunika nyuso zao na barakoa, waliwajibu polisi hao kwa kuwatupia mabomu ya petrol.
Wanafunzi wa Haiti nao hawakuwachwa nyuma,wanafunzi wa shule za sekondari walimiminika na kuwaunga mkono walimu wao waliogoma kwa sababu ya mishahara midogo.Polisi wa Haiti pia walitumia gesi za machozi kuwatawanyisha waandamanaji hao.
Serikali ya Haiti imewahimiza walimu kurudi darasani mpaka bajeti mpya itakapopitishwa bungeni. Uamuzi  wa kuwaongezea mishahara bado inajadiliwa bungeni.

No comments: