Rais wa Marekani Barack Obama atasafiri kwenda Poland, Ubelgiji na Ufaransa mwezi wa Juni.
Kutokana na taarifa ya maandishi kutoka
White House, Obama atafanya mazugumzo baina ya nchi katika mji mkuu wa
Poland Warsaw, na yeye pamoja na viongozi wengine wa dunia watahudhuria
kumbukumbu ya kuadhimisha miaka 25 ya mwisho wa ukomunisti nchi Poland.
Baada ya Poland Obama atazuru Brussels
ambapo atahudhuria mkutano wa G-7 utaofanyika kati ya Juni tarehe 4-5.
Katika mkutano huo ajenda kuhusu uchumi, usalama na maendeleo
itaongelewa na viongozi hao huku majadiliano kuhusiana na swala la
Ukraine yaliyofanywa Hague mwezi Machi tarehe 24 kuendelezwa.
Mkutano wa G-8 uliopangwa kufanywa katika
mji wa Sochi nchini Urusi ulisitishwa baada ya Urusi kujiunga na Crimea
na mkutano huo kukubaliwa kufanywa Brussels kama G-7.
Baada ya Brussels Obama atazuru Ufaransa na hapa atahudhuria kumbukumbu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Normandy.
No comments:
Post a Comment