Friday, 2 May 2014

Serikali ya Malaysia yaomba muda zaidi wa uchunguzi

Serikali ya Malezya imeziomba familia za abiria wandege iliyopotea kurejea nyumbani na kungoja habari kutoka kwa serikali.

serikali-ya-malaysia-yaomba-muda-zaidi-wa-uchSerikali ya Malezya imeziomba familia za abiria wandege iliyopotea kurejea nyumbani na kungoja habari kutoka kwao.
Shughuli za kutafuta ndege hiyo ambayo ilipotea tarehe 8 mwezi Mei zimefikia hatua nyingine. Shughuli za kutafuta ndege hiyo Magharibi mwa Australia kwa kutumia kifaa cha rada hazikufanikiwa kuipata ndege hiyo. Uchunguzi katika eneo hilo lililokuwa limetengwa kwa ajili ya uchunguzi umemalizika bila mafanikio yoyote.
Uchunguzi wa kutafuta ndege hiyo angani pia ulimalizika baada ya kugharimu mamilioni ya dola za Amerika. Uchunguzi wa kutafta ndege hiyo katika sakafu ya bahari utakaoongozwa na waziri mkuu wa Australia Tony Abbott zitaendelea kwa kipindi cha kati ya miezi 6 mpaka 8.
Malezya iliwasilisha ripoti kuhusiana na kutoweka kwa ndege hiyo kwa Shirika La Kimataifa La Anga. Kulingana na ripoti hiyo kupotea kwa ndege hio kulijulikana baada ya dakika 17 kwani ilikuwa imeingia katika anga ya Vietnam. Ripoti hiyo ilipendekeza kuwekwa kwa mfumo wa kutambuo eneo la ndege angani.
Shirika moja la Australia linadai kuwa ndege hiyo ipo katika sakafu ya bahari huku Rubani mmoja wa kiamerika anayehusika na utathmini wa picha za satellite akidai kuwa ndege hiyo ipo magharibi mwa nchi ya Thailand.

No comments: