Friday, 12 June 2015

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa Bw. Said Djinnit amejiuzulu nafasi ya upatanishi kwenye mgogoro wa Burund

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa Bw. Said Djinnit amejiuzulu nafasi ya upatanishi kwenye mgogoro wa Burundi baada ya kulalamikiwa na upinzani nchini humo kwa kuwa na upendeleo.
Bw. Djinnit ataendelea kuwa mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kwenye kanda ya Maziwa Makuu. Upinzani umemlaani Bw. Djinnit kwa kupendelea upande wa serikali ya Burundi kwenye mazungumzo ya pande mbili kuhusu mgogoro uliotokana na rais Pierre Nkurunziza kutaka kuwania urais kwa awamu ya tatu. Bw. Djinnit amekanusha lawama hiyo.
Habari nyingine kutoka Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa zinasema, zaidi ya wakimbizi 7,700 wa Burundi wameingia Uganda kuanzia mwezi Novemba mwaka jana, na tangu tarehe mosi mwezi huu kila siku kuna takriban wakimbizi 144 wanaomiminika nchini Uganda kutoka Burundi.

No comments: