Bi. Rehema Gwaya ambaye amelazwa katika Hospitali ya mkoa Songea
akiwa na mwanae wa miezi saba anasema chanzo cha kufanyiwa ukatili huo
ni kutofautiana na mke mwenzake aitwaye Zefania Chimgege baada ya kuhoji
masuala ya usafi ambapo zefania aliyekuwa akipika maandazi akamwagia
karai la mafuta ya moto usoni.
Baada ya kufanyiwa unyama huo shemeji yake ambaye ni mume wa
Zefania Bw.Hafidhi Hamidu Mbaya akamwambia atoke nje ammalizie kwa
kumchoma na kisu.
Mganga mfawidhi katika hospitali ya mkoa Songea(HOMSO) Dkt.Benedikt
Ngaiza anaelezea hali ya mgonjwa huyo huku wakazi wa songea wakilaani
ukatili huo.
Rehema Gwaya na Zefania Chimgege wameolewa sehemu moja na wote
wanaishi katika nyumba ya baba Mkwe na waume zao na kwamba zefania
chimgegeanashikiliwa na polisi kwa kufanya ukatili huo.
No comments:
Post a Comment