Kenya iliandaa sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya kujitawala siku ya Jumatatu katika mji mkuu wa Nairobi.
Sikukuu ya Madaraka ilihudhuriwa na rais wa nchi Uhuru Kenyatta pamoja na viongozi wengine wa ngazi za juu serikalini.
Viongozi wa nchi mbalimbali za Afrika kama vile rais wa Uganda Yoweri Museveni na makamu wa rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa pia walihudhuria sherehe hiyo.
Kulikuwa na hafla mbalimbali zilizoandaliwa ikiwa ni pamoja na magwaride ya vikosi vya walinzi wa usalama nchini Kenya.
Akitoa hotuba katika sherehe hiyo ya maadhimisho, Uhuru Kenyatta alihimiza halmashauri zote nchini kupambana dhidi ya ufisadi, na kuchukuliwa hatua kali kwa watu wanaohusika na kesi za kula rushwa wakiwemo viongozi.
Uhuru Kenyatta pia alisema kwamba serikali yake inajiandaa kuimarisha usalama na kupunguza janga la umaskini nchini Kenya.

No comments:
Post a Comment