Daktari
wa usapuaji nchini Afrika Kusini amethibitisha kwamba mwanamme wa
kwanza aliyepandikizwa uume atakuwa baba hivi karibuni.
Professor
Andre van der Merwe, ambaye ndiye aliyefanya upasuaji huo mwezi Disemba,
ameiambia BBC kwamba mwenza wa mgonjwa huyo ana uja uzito wa miezi
minne.Mwanamme huyo mwenye umri wa miaka 21 alipoteza uume wake pindi alipokuwa anapashwa tohara ambayo haikufanikiwa.
Professor van der Merwe ameendelea kusema habari hizo zinaonyesha kuwa upandikizwaji huo wa kiungo umefanikiwa kabisa na unaweza kufanyiwa wagonjwa wengine katika siku zijazo.
No comments:
Post a Comment