Friday 5 June 2015

Gatlin avunja rekodi ya Bolt

Gatlin
Mwanariadha wa Marekani Justin Gatlin ameishinda rekodi ya Usain Bolt na kuweka rekodi mpya katika mbio za Diamond League za mita 100.
Gatlin mwenye umri wa miaka 33 aliwaongoza wenzake na kushinda kwa sekunde 9.75 ikiwa ni mda bora wa saba kuwekwa katika historia na hivyobasi kuipiku rekodi ya Bolt ya sekunde 9.76 iliowekwa mwaka wa 2012.
Gatlin ambaye amehudumia marufuku ya kutumia dawa za kusisimua misuli alikimbia mda wa sekunde 9.74 katika mkutano wa kwanza wa mbio za Diamond League mwezi uliopita.
Bingwa wa mbio za Olimpiki Sally Pearson alipata jeraha la kifundo cha mkono baada ya kuanguka katika mbio za kuruka viunzi za mita 100 upande wa wanawake.

No comments: