Waziri wa fedha na uchumi Mhe.Saada Mkuya amesema hukusanyaji huo
wa mapato yasiyo ya kodi utahusisha faini za mahakamani, faini za
usalama barabarani, viingilio katika mbunga za wanyama, vibali vya
kuvuna maliasili na kuwataka maafisa masuhuli kusimamia utekelezaji wa
agizo hilo na kusisitiza mpango huo utasaidia kupunguza utegemezi wa
fedha za wahisani.
Aidha amesema serikali imependekeza kuongeza tozo kwenye mafuta ya
taa kutoka shilingi 50 kwa lita hadi shilingi mia moja hamsini kwa lita
ili kuondoa uchakachuaji wa mafuta ambapo amesema kuwa hatua ya kuongeza
tozo katika mafuta ya Petroli zinalenga kuongeza mapato ambayo
yataelekezwa katika mradi wa usambazaji umeme vijijini.
Akielezea shabaha ya msingi ya bajeti ya mwaka 2015/16 Mhe.Mkuya
amesema kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani ikijumuisha mapato ya
serikali za mitaa kufikia asilimia 13.1 ya pato la taifa ambapo matumzi
ya serikali yanatarajiwa kuwa asilimia 20.6 ya pato la taifa na kuwa
akiba ya fedha za kigeni kwa kiwango cha kukidhi matumizi ya bidhaa na
huduma.
Aidha amesema katika bajeti ya mwaka 2015/16 inavipaumbele vichache
ikiwemo kugharamia uchaguzi mkuu pamoja na gharama zote za bunge
lijalo, kuweka msukumo katika miradi inayoendelea kwenye miradi ya umeme
na maji vijijini na kuimarisha rasilimali watu.
No comments:
Post a Comment