Mmoja
kati ya watu wanaowania kuteuliwa na chama cha mapinduzi kugombea urais
wa jamhuri ya muungano Mhe.Steven Wasira amewataka watangaza nia wenzake
kuacha siasa za kuchafuana bali wafanye siasa za kuwaeleza watanzania
watawafanyia nini iwapo watachaguliwa.
Mhe.Wassira amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na
watu ambao wamejitokeza kumdhamini na kuongeza kuwa matatizo sugu ya
watanzania kama mapambano dhidi ya rushwa ndiyo yanayopaswa kujadiliwa.
No comments:
Post a Comment