Marekani
imetumia zaidi ya dola bilioni mbili unusu katika kufadhili vita dhidi
ya Islamic State, kupitia kutekeleza mashambulizi ya angani nchini Iraq
na Syria tangu mwezi Agosti mwaka jana.
Makao makuu ya Pentagon
yametoa orodha ya gharama ya fedha zilizotumika, inayoonyesha kuwa
inatumia zaidi ya dola milioni tisa kwa siku katika kutekeleza
operesheni hiyo.Bunge la Marekani limekataa jaribio la kuzuia matumizi zaidi ya fedha ili kukabiliana na IS.
Bunge la wawakilishi limepitisha mswaada wa kuikubalia wizara ya ulinzi kutumia dola bilioni mia tano na themanini.
No comments:
Post a Comment