Cristiano Ronaldo alielezea kuchoshwa kwake na tabia ya kufuatwafuatwa na “mapaparazi” ambao wamekuwa wakimfuata akiwa likizoni.
Ronaldo alisema kuwa nia yao ni kumchafulia jina kwa kumhusisha na wanawake wapya kila wiki huku wakisingizia kuwa alikuwa mtu wa kubadilisha wanawake.
Katika ujumbe wake kwa waandishi wa habari aliteta, “Niwacheni huru. Katika wiki zilizopita habari mbalimbali za kuniharibia jina zimekuwa zikisambazwa pande zote. Nipo likizoni, napumzika na mwana wangu yupo pamoja nami. Niwacheni huru, niwacheni kama ilivyo ada ya kila mwaka nifanye kazi yangu. Wacheni kujaribu kuniharibia sifa kwani katika hilo hamtafanikiwa.”
Ronaldo pia alitoa shukrani kwa mashabiki wake kwa kuwa pamoja naye katika msimu huu mgumu

No comments:
Post a Comment