Waokoaji wanajaribu kufukua udongo ili kuwanusuru watu waliozikwa .
Takriban mashine saba za kufukua udongo zimekuwa zikihusika katika shughuli ya uokozi katika mgodi huo ulioko kusini magharibi mwa sehemu ya Cauca.
Kando kando mwa mgodi huo wapo mamia ya jamaa na marafiki ya wachimba migodi waliofukiwa ambao wanafuatilia kwa karibu shughuli za uokoaji.
Lakini mmoja wa wazima moto amesema kuwa hamna matumaini makubwa
"Hakuna matumaini , kwani sidhani kuna uwezo wa mtu kusalia hai baada ya kufunikwa na matope haya kwa muda huu wote pasi na hewa "
Amesema serikali yake inapigana vita dhidi ya uovu huo.
Lakini mwandishi wa BBC ameongezea kuwa kuna migodi kadhaa katika maeneo fiche nchini humo.
Ijumaa wiki iliyopita, wachimba migodi wengine wanne walipoteza maisha yao huku sitini na tano wengine wakiathirika na gesi ya sumu katika sehemu ya Antioquia
No comments:
Post a Comment