VIJANA
zaidi ya 1,000 ambao ni wanachama wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha
Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Meru, Mkoa wa Arusha, wamevamia ofisi za
chama hicho kuanzia ngazi ya wilaya na mkoa, wakidai wamechoshwa na
uongozi wa juu wa chama kuwachagulia viongozi ambao si chaguo lao.
Vijana hao walidai viongozi waliopo makao makuu ya chama hicho wamewaonea kwa kutangaza uamuzi wao wa kuwachagulia viongozi tofauti na matakwa yao.
Alisema wao walimchagua Kamanda wao, John Palangyo, lakini uongozi wa CCM makao makuu walitofautiana nao.
Maandamano hayo ambayo yaliratibiwa na wajumbe wa UVCCM Meru, yalisababisha shughuli mbalimbali za chama hicho kuanzia ofisi ya wilaya hadi mkoa kusimama kutokana na baadhi ya vijana hao kulazimika kuingia kwa nguvu ndani ya ofisi hizo, kisha kushinikiza kusikilizwa kwa madai yao.
Akizungumza kwa niaba ya wajumbe hao mmoja wa wajumbe hao, Joshua Mbwana, alisema kilichosababisha wafanye maandamano hayo ambayo yalianzia Usa River Arusha ni kuelezea umma kuwa wapo baadhi ya viongozi katika chama hicho ambao wanawachagulia viongozi wa kuwaongoza bila kuwauliza.
“Hivi juzi tulimchagua kamanda wetu ambaye ni John Palangyo na tulimpitisha, lakini baada ya jina kufika mkoani ghafla jina lilibadilishwa kama haitoshi makao makuu wakasema kuwa wana mtu wao... sasa je, wao ndio wanatuchagulia mtu wa kutuongoza au sisi? Kamwe hatutakubali na badala yake tutapigana hadi mwisho hii tabia imetuchosha sana,” alisisitiza Joshua.
Alidai endapo hali hiyo itaendelea kufanyika mapambano yatakuwa makubwa sana.
Alisema pamoja na kuwa wamevamia ofisi za CCM; kama hawatapewa majibu ya kuridhisha ndani ya siku nne kuanzia sasa huenda wakaandamana hadi makao makuu ya ofisi za CCM.
“Tumesharatibu maandamano hayo, maandalizi yanaenda vizuri itakuwa ni historia kwa CCM kutuchagulia viongozi kwa masilahi yao binafsi na matakwa ya viongozi wa ngazi za juu hasa wale ambao wana malengo ya kugombea nafasi za ubunge katika majimbo yao,” alisema na kuongeza;
“Ujumbe wetu ni lazima tutauweka wazi na kila mtu aweze kusoma, lakini hata kuingia ndani ya ofisi hizo bila taarifa wala kibali cha aina yoyote ile,” alisema.
Katibu wa CCM Wilaya ya Meru, Langaeli Akyoo, alisema kuwa mchakato wa kumpata kiongozi ambaye vijana hao wanamtaka ulienda vizuri na majina matatu yalifikishwa Dar es Saalam makao makuu ya chama, lakini baadaye hayakurudi kama ilivyotarajiwa.
Akyoo alisema majina mawili yalirudi, lakini majina mawili ambayo yana utata mkubwa ndiyo yalisababisha maandamano makubwa kuanzia Meru hadi Arusha.
“Jamani maombi yenu nimeyapata na ninapenda kuwaambia kuwa majina ambayo yalienda Dar es Salaam makao makuu yalirudishwa mawili ambayo yana utata na wao walisema kuwa mchakato unatakiwa kuanza moja jambo ambalo sisi hatukubaliani nalo kabisa,” alisema Akyoo.
Awali, mwenyekiti wa umoja wa vijana wilaya hiyo, Bw Elirehema Mbisse alisema kuwa, mchakato wa kumpata Kamanda huyo unaendelea na hivyo amewataka wawe na subira ili waweze kuangalia namna ya kutatua tatizo hilo ambalo limesababisha ofisi za CCM kusimamisha kazi kwa muda.
Uongozi wa UVCCM kupitia kikao chake cha kamati ya utekelezaji kilipendekeza majina matatu ambayo ni John Palangyo, Sioi Sumari na Daniel Palangyo.
Baada ya miniti kupelekwa mkoani ambapo mkoa ulijiridhisha na majina hayo na uliweza kuhoji na hatimaye waliweza kumpata John Palangyo kama Kamanda wa Vijana Wilaya ya Meru,lakini baadaye barua ilikuja na kudai kuwa kamanda wa Meru si huyo jambo ambalo si la kweli.

No comments:
Post a Comment