Mwanzo mzuri: James Wilson aliifungia Man United mabao mawili katika mechi yake ya kwanza usiku huu.
MANCHESTER United wamemaliza mechi za Old Traffod kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Hull City usiku huu.
Kocha
mkuu wa muda wa Man United, Ryan Giggs katika mchezo wa leo aliamua
kuwapa nafasi wachezaji vijana wa klabu hiyo Tom Lawrence na James
Wilson.
Pia Michael Keane alikaa benchi tayari kwa kuwaonesha kazi Hull.
Wilson
mwenye miaka 18 mapema aliwaaminisha mashabiki wa Man United kuwa
anaujua mpira baada ya kuifungia bao katika dakika ya 31, na baadaye
dakika ya 61 aliandika bao la pili kimiani kabla ya mkongwe Robin Van
Persia kufunga bao la tatu katika dakika ya 86.
Bao la Hull limefungwa katika dakika ya Fryatt dakika ya 63.
Kijana huyo wa ajabu ni nani?
Umri: 18
Alipozaliwa: Staffordshire
Mechi za kwanza: Wilson
anapenda mechi za kwanza. Mshambuliaji huyo alifunga bao katika mechi
yake ya kwanza kwenye akademi ya Man United ya miaka 15.Pia alifunga bao
lake la kwanza kwenye mechi yake ya kwanza katika kikosi cha timu ya
taifa ya England chini ya miaka 19 mwaka 2013.
Ukweli wa kufurahisha: Wilson alisaini mkataba wa kitaaluma na Man United siku yake ya kuzaliwa ya mwaka wa 17 mwaka 2012.
Ryan Giggs alishinda mataji mawili ya ligi, moja la FA na kombe moja la ligi kabla ya Wilsom kuzaliwa.
Ukweli wa kufurahisha: Wilson alisaini mkataba wa kitaaluma na Man United siku yake ya kuzaliwa ya mwaka wa 17 mwaka 2012.
Wilson (kulia) akishangilia bao lake na Nemanja Vidic |
Ryan Giggs alishinda mataji mawili ya ligi, moja la FA na kombe moja la ligi kabla ya Wilsom kuzaliwa.
James Wilson
Akiwa
na miaka 15, Wilson alifunga bao lake la kwanza katika mchezo wa kwanza
dhidi ya Everton na ikiwa imepita miaka mitatu sasa amefanya kitu kama
hicho tena, lakini safari hii amefunga katika mechi yake ya kwanza
kwenye mchezo wa ligi kuu.
Giggs
amempatia nafasi kijana huyo mwenye miaka 18 kucheza mechi yake ya
kwanza na ameweza kuwaaminisha Man United kuwa anajua soka baada ya
kufunga bao kipindi cha kwanza.
Mashabiki
wa United walimfahamu mshambuliaji huyu kijana siku alipowekwa benchi
na Moyes kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Newcastle mwezi aprili mwaka
huu, wakati huo wote Rooney na Van Persie hawakuwepo.
Wilson hakuingia uwanjani, lakini aliwashangaza wengi kwa kupangwa kwake katika mechi kubwa kama hiyo.
Cha
kufurahisha, Wilson aliamua kuvaa soksi na viatu vyeuusi katika mechi
yake ya kwanza Old Trafford usiku huu, kitu ambacho si cha kawaida kwa
soka la sasa ambapo wachezaji wengi wanapenda kuvaa viatu na soksi za
rangi.
Mtoto wa shule: Tofauti na vijana wa soka la kisasa siku hizi, Wilson aliingia uwanjani akiwa na viatu vyeusi.
No comments:
Post a Comment