Thursday, 8 May 2014

ubingwa wanukia ETIHADI . MAn city yanyuka Aston Villa 4 0

Man of the hour: Edin Dzeko roars to the Etihad stands after his first goal gives City the lead
Mtu wa heshima: Edin Dzeko akiunguruma baada ya kufunga bao lake la kwanza leo Etihad dhidi ya Aston Villa.
KWA asilimia kubwa mnuso wa ubingwa wanukia Etihad baada ya Manchester City kuibuka na ushindi mtamu wa mabao 4-0 dhidi ya Aston Villa katika mchezo wa ligi kuu soka nchini England.
Ushindi huu umewarejesha Man City kileleni na sasa wanahitaji pointi moja tu kutwaa taji msimu huu.
Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika kwa milango ya timu zote kuwa migumu.
Baada ya kuingia katika vyumba vya kuvalia nguo, Manuel Pellegrini aliwakumbusha vijana wake kuwa wamebakiwa na kazi ndogo kuchukua taji.
Man City waliporudi kipindi cha pili walikuja na kasi nzuri na katika dakika ya 64 na 72, Edin Dzeko alifunga mabao mawili.
Wakati Aston Villa wakitafuta njia ya kusawazisha, katika dakika ya 89, Stefan Jovetic aliifungia bao la tatu Man City.
Dakika ya 93, mwafrika mwenye kiwango cha juu zaidi, Yaya Toure alihitimisha karamu ya mabao na kuwafanya City wakaribie kuutwaa ubingwa wa pili ndani ya misimu mitatu.
City wameishusha Liverpool kileleni kwa kufikisha pointi 83, huku Liverpool wakibakia nafasi ya pili kwa poini 81. Timu zote zimecheza mechi 37. 
Sare ya mabao 3-3 waliyopata Liverpool jumatatu ya wiki hii dhidi ya Crystal Palace imewafanya wawe katika wakati mgumu wa kufuta ukame wa miaka 24 bila kombe, na sasa wanawaombea dua mbaya Man City wafungwe mechi ya mwisho siku ya jumapili dhidi ya West Ham kwenye uwanja wa Etihad.
And now you've gotta believe us: Dzeko is joined by his City team-mates to celebrate his second goal
Dzeko akiungana na wachezaji wa Man City kushangilia bao lake la pili.
 
Kikosi cha Man City leo: Hart, Zabaleta, Kompany, Demichelis, Kolarov, Javi Garcia, Toure, Milner, Silva, Nasri, Dzeko.
Wachezaji wa akiba: Richards, Lescott, Negredo, Clichy, Fernandinho, Pantilimon, Jovetic. Kikosi cha Aston Villa: Guzan, Lowton, Vlaar, Baker, Clark, Bertrand, El Ahmadi, Westwood, Delph, Weimann, Bowery. Wachezaji wa akiba: Bacuna, Steer, Sylla, Tonev, Holt, Robinson, Grealish. Mwamuzi: Michael Oliver
Acrobatic: City captain Vincent Kompany attempts an audacious overhead kick
Vitu vya hatari vya nahodha wa Man City Kompany
On strike: Villa forward Andreas Weimann (right) shoots past City's Pablo Zabaleta
Shuti kali: Mshambuliaji wa Villa Andreas Weimann (kulia) akiachia shuti kali lililompita beki wa City Pablo Zabaleta
Can't even watch: Manuel Pellegrini can barely look with his side on the brink of a Premier League title
Hataki kutazama: Manuel Pellegrini yupo katika asilimia kubwa ya kutwaa taji la ligi kuu.
Lining up: Aleksandar Kolarov attempts to hit a free-kick past the Aston Villa wall
Aleksandar Kolarov akipiga mpira wa adhabu ndogo
Making his point: Paul Lambert shouts instructions to his side from his technical area
Zuia kule bwana wewe!: Kocha wa Aston Villa, Paul Lambert akitoa maelekezo kwa wachezaji wake
Near miss: A frustrated Samir Nasri misses from close range for Manchester City
Almanusura apige vitu: Samir Nasri alikosa nafasi nzuri ya kuifungia bao Manchester City
Battle: Goalscorer Dzeko (left) challenges Aston Villa's Karim El Ahmadi
Vita: Mfungaji mkali,  Dzeko (kushoto) akichuana na beki wa Aston Villa, Karim El Ahmadi
Signs are there: One cheeky City fan won't let Steven Gerrard forget his crucial slip against Chelsea Ishara nazo zipo: Shabiki mmoja wa Man City  akionesha bango la kumkejeli  Steven Gerrard
Pleading: Joe Hart reacts as his side move within inches of the Premier League title
Maombi kwa sana: Joe Hart akiomba baada ya timu yake kukaribia kutwaa ubingwa wa ligi kuu. Katika mchezo mwingine, maajabu ya soka yameendelea kutokea kwa Sunderland baada ya usiku wa leo kushinda mabao 2-0 dhidi ya West Brom.
BAADA YA MECHI ZA LEO MSIMAMO WA EPL KWA TIMU 10 ZA JUU HUU HAPA

English Barclays Premier League | LOGS

Pos Team P W D L GF GA GD Pts
1 Manchester City 37 26 5 6 100 37 63 83
2 Liverpool 37 25 6 6 99 49 50 81
3 Chelsea 37 24 7 6 69 26 43 79
4 Arsenal 37 23 7 7 66 41 25 76
5 Everton 37 20 9 8 59 39 20 69
6 Tottenham Hotspur 37 20 6 11 52 51 1 66
7 Manchester United 37 19 6 12 63 42 21 63
8 Southampton 37 15 10 12 53 45 8 55
9 Newcastle United 37 15 4 18 42 57 -15 49
10 Stoke City 37 12 11 14 43 51 -8 47

No comments: