Ilielezwa mahakamani hapo jana kuwa kesi hiyo
haiwezi kusikilizwa kwa sasa kwa kuwa jalada lake bado halijarudi kutoka
Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam.
Sheikh Ponda anakabiliwa na mashtaka matatu ambayo
ni kutotii amri halali ya iliyotolewa na Mahakama ya Kisutu, kutoa
maneno yenye kuharibu imani za dini na kushawishi watu kutenda kosa,
makosa ambayo anadaiwa kuyatenda Agosti 10 mwaka jana katika eneo la
Uwanja wa Ndege Manispaa ya Morogoro.
Baada ya kutajwa kwa kesi hiyo, Hakimu Mkazi
Mfawidhi Mary Moyo alisema kesi hiyo itaendelea kutajwa mpaka jalada
hilo lililoitishwa Mahakama Kuu Oktoba 15 litakaporudishwa Mahakama ya
Morogoro.
Sheikh Ponda alifikishwa mahakamani hapo jana
chini ya ulinzi mkali wa polisi waliokuwa na sihala za moto, mabomu ya
machozi na mbwa huku wafuasi wake wakizuiwa nje ya uzito wa mahakama
hiyo.
Upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Wakili wa
Serikali, Lilian Lutabula aliyeshirikiana na mwendesha mashtaka wa
polisi, Zabron Msusi wakati upande wa utetezi uliwakilishwa na wakili
Josephine Jackson kwa niaba ya wakili Bathoromeo Tarimu anayemtetea
Sheikh Ponda.
Baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, mshtakiwa
Ponda alirudishwa rumande ambako ataendelea kupafanya kuwa maskani yake
hadi Mei 5 mwaka huu kesi hiyo itakapoendelea kutajwa mahakamani hapo.
No comments:
Post a Comment